WAZIRI Mkuu Afuta Posho zote kwa Watumishi wa Umma Nchini

Serikali ya awamu ya tano imeendeleza desturi yake ya kubana matumizi, ambapo leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefuta rasmi posho zote za watumishi wa Umma na kuelekeza posho hizo kufanyiwa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri husika nchini.
Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo leo 3 Januari 2017, katika ziara yake iliyofanyika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akieleza jambo hilo amebainisha:“Kuanzia Januari hii mtu asipewe posho ya aina yoyote ile, nafuta posho zote ziende katika miradi ya maendeleo,”amesema Majaliwa.
Aidha, Waziri Majaliwa ameagiza Halmashauri zote nchini kusimamia fedha za miradi ya maendeleo za madiwani.

“Sasa hivi madiwani hakuna kupewa fedha za miradi ya maendeleo mkononi, bali wawasilishe vipaumbele vya miradi yao ili halmashauri husika isimamie malipo yake kwa ajili ya kuepuka migogoro,”amesema.
Pia, Majaliwa amezipiga marufuku kampuni za watumishi wa umma kufanya kazi katika halmashauri wanazofanyia kazi.

“Madiwani kama mna kampuni haziruhusiwi kufanya kazi katika halmashauri walizopo ili kuondoa upatikanaji wa dhabuni za upendeleo kitendo kinachoshusha ufanisi wa kazi,”amesema.
Amezitaka halmashauri zote nchini kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya kodi na yasiyo ya kodi.
”Serikali itaendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kwa halmashauri zote nchini kulingana na bajeti itakavyo ruhusu, tunataka halmashauri zitekeleze miradi yake ipasavyo,”amesema.

Amesema kwa sasa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam zinateketeza fedha nyingi kwa ajili ya posho badala ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo Halmashauri za wilaya ya Temeke na Kigamboni zinatumia laki 5 kila mwezi kwa ajili ya posho za kuchochea maendeleo ya madiwani
wakati Ubungo ikitumia milioni 55 ambayo ni sawa na zaidi ya milioni 600 pamoja na posho za vitafunwa milioni 300 kwa mwaka huku Kinondoni ikitumia milioni 780 kwa ajili ya posho ya maendeleo na milioni 390 kwa ajili ya posho ya bites kila mwaka.

JF
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu ndiyo uwajibikaji tunao utaka sisi watanzania. na imani juu yenu tunayo. nia zenu mungu awasaidie ni njema. tunakuombe Mh Majaliwa Allah akupe afya njema na umuri mrefu ili uendelee kwa kasi hii hii kumsaidia na kushiriliana na Mh JPJM Kutuletea Tanzania mpya tunayo itaka. chonde chonde BUNGE NA MALIPO YA KIPUNGUANI yanahitaji mapitio. HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. Huu ndiyo uwajibikaji tunao utaka sisi watanzania. na imani juu yenu tunayo. nia zenu mungu awasaidie ni njema. tunakuombe Mh Majaliwa Allah akupe afya njema na umuri mrefu ili uendelee kwa kasi hii hii kumsaidia na kushiriliana na Mh JPJM Kutuletea Tanzania mpya tunayo itaka. chonde chonde BUNGE NA MALIPO YA KIPUNGUANI yanahitaji mapitio. HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  3. Yaani watu walijua kujipatia ndio maana kila mmoja wao ana kifriza cha maradhi sasa mtaijua namba n.a. zile gari zenu zitafungiwa uani shuwaini kazi miaka miwili holiday Dubai familia nzima

    ReplyDelete
  4. Huuu ndio Uongozi na uwajibikaji kazini, ukisikia IQ intergent Qulity ndio awamu hii ya viongozi, yaani ni viongozi wanaojielewa katika nchi hii kama si bara hili la Africa, kwa maana ni wachache sana

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad