WAZIRI wa Burundi apigwa risasi na kufariki siku ya mwaka mpya

Wakati dunia ikisherehekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2017, nchi ya Burundi imeingia kwenye majonzi baada ya kumpoteza Waziri wake wa Mazingira aliyefariki kwa kupigwa risasi saa chache baada ya kuukaribisha mwaka mpya.

Jeshi la polisi la nchi hiyo limedai kuwa waziri huyo amepigwa risasi wakati akielekea nyumbani kwake huko Rohero. Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza ameahidi kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayefahamika kuhusika na mauaji hayo.

Hili ni tukio la kwanza nchini humo kuuawa kwa kiongozi wa serikali lakini tayari wameshawahi kuwapoteza maafisa kadhaa kutoka kwenye jeshi la nchi hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad