STAA wa filamu za Bongo, Jackline Wolper, amesema sasa hivi ameamua
kuanza maisha ya kistaa kwa kutoanika mambo yake binafsi kwenye mitandao
ya kijamii, kwani aliyokuwa anafanya mwanzo ilikuwa ni ushamba.
Akizungumza , Wolper alisema kwa muda mrefu ameishi
maisha ya kishamba kwa kuanika mambo yake binafsi kwenye mitandao badala
ya kuitumia kutangaza kazi zake za filamu.
“Kiukweli sasa nimeelimika na nimejijua kama mimi ni staa na
ninapaswa kuishi kistaa, sitarusha chochote kile kinachohusu maisha
yangu kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Wolper.
Msanii huyo alisema mastaa wa Kibongo wamekuwa washamba na mitandao
hiyo kwani wameshindwa kuitumia kibiashara kama wanavyofanya wenzao
kutoka nchi nyingine duniani.
yeye mwenyewe mshamba.
ReplyDelete