Serikali ilitangaza kuwa ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa utaanza mwezi
Disemba mwaka jana kwa msaada kutoka nchi ya China. Leo ni mwezi Januari
hata zabuni ya kampuni iliyoshinda kutekeleza mradi huo Serikali
haijatangaza. Hata hivyo tumesikia kuwa kampuni kutoka Uturuki imeshinda
zabuni hiyo na China (ambao ndio watoa mkopo wa mradi husika)
wamekasirika na wamegoma kutoka fedha zao.
Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa Uturuki anakuja nchini wiki ijayo. Hatukatai kuimarisha mahusiano na Uturuki, lakini ni muhimu Serikali ijitazame upya kuhusu mahusiano yake na China. China ni rafiki wa Tanzania wa misimu yote. Tanzania imekuwa na China muda wote na China imekuwa na Tanzania muda wote. Maamuzi ya Serikali ya kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo yanaweza kugharimu sana mahusiano yetu ya zaidi ya miaka 50.
Tunamsihi Rais awe makini sana na mwenendo wake wa kutojali misingi imara ya Sera yetu ya mambo ya nje. Serikali ikae chini na China kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo hatutajenga Reli hiyo, ama itachukua miaka mingi sana kuijenga Reli hiyo. Madhara ya kuchelewa kujenga Reli ya Kati ni makubwa mno kwani washindani wetu wa kibiashara, Kenya, wanamaliza Reli yao sasa kuunganisha na nchi za Rwanda na Mashariki ya Kongo.
Namkumbusha Rais na Serikali namna ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani walivyovunja misingi yetu kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje, hasa kuhusu Sahara Magharibi na Mashariki ya Kati. Tumeikumbatia Moroko kwa ahadi ya viwanja vya mipira na misikiti na kuwaacha wananchi wa Sahara Magharibi ambao Mwalimu Nyerere aliwalinda kwa gharama zote. Juzi juzi kwa mara ya kwanza tumewasaidia Israel kwenye Umoja wa Mataifa bila ya kujali msimamo wetu wa 'Two States Solution' kati ya Palestine na Israel.
Sasa tunakwenda kuweka nyufa kwenye mahusiano yetu na China. Serikali ijitazame upya. Tanzania haikuanza na awamu ya Tano, nchi hii imekuwapo na itaendelea kuwapo. Hatuwezi kukaa kimya tukiendelea kuona misingi ya nchi yetu inavunjwa vunjwa. Lazima tukemee.
"Hata hivyo tumesikia kuwa kampuni kutoka Uturuki imeshinda zabuni hiyo na China (ambao ndio watoa mkopo wa mradi husika) wamekasirika na wamegoma kutoka fedha zao."
ReplyDeleteKwanza hiki kitu cha tumesikia kinatoka wapi????......Kama kweli ni reliable information ni kwa nini kuwepo na neno kusikia.
Kuhusiana na China kuwa wamekasirika na pia wamegoma kutoa pesa zao(Kama ni kweli) simply because hawakushinda hiyo zabuni na hiyo zabuni ni kampuni ya Uturuki imeshinda, je jambo la kujiuliza ni kuwa huo msaada wa pesa za ujenzi wa Reli ya Kati kutoka China zilikuwa na masharti ama zilikuwa hazina masharti. Na je moja ya hayo masharti ilikuwa ni lazima kwa kampuni ya ujenzi wa hiyo Reli ya kati itoke pale China?????......Na kama ni hivyo,je kulikuwa na maana gani ya kuitisha zabuni???? Hiyo zabuni ilikuwa ya nini na iliitishwa kwa misingi gani.
"Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa Uturuki anakuja nchini wiki ijayo. Hatukatai kuimarisha mahusiano na Uturuki, lakini ni muhimu Serikali ijitazame upya kuhusu mahusiano yake na China. China ni rafiki wa Tanzania wa misimu yote. Tanzania imekuwa na China muda wote na China imekuwa na Tanzania muda wote. Maamuzi ya Serikali ya kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo yanaweza kugharimu sana mahusiano yetu ya zaidi ya miaka 50."
ReplyDeleteKatika kipengele na melezo aliyoyatoa huyo Bwana Zitto Kabwe kuhusiana na mahusiano kati ya Tanzania na China pamoja na ziara itakayofanywa na Rais wa Uturuki kinatia wasiwasi. Swali la kujiuliza hapa je ni kweli hiyo ziara itakayofanywa na Rais wa Uturuki hapo Tanzania inakiuka na kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo????......Na je ni kweli hiyo ziara itakayofanywa na Rais wa Uturuki hapa Tanzania italigharimu Taifa la Tanzania mahusiano yake na China ambayo yamedumu kwa kipindi cha miaka 50??????? (Kwa mujibu wa huyo Zitto Kabwe).
"Tunamsihi Rais awe makini sana na mwenendo wake wa kutojali misingi imara ya Sera yetu ya mambo ya nje. Serikali ikae chini na China kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo hatutajenga Reli hiyo, ama itachukua miaka mingi sana kuijenga Reli hiyo."
ReplyDeleteSasa huyu Bwana Zitto Kabwe hatuelezi ni kwa kiasi gani Rais wetu haijali na wala hazingatii ile misingi imara ya sera za mabo ya nje. Halafu anaendelea kwa kusema na kumsisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akae chini na China ili kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo haitajengwa ama itatuchukua muda mrefu kuijenga.(Kwa mujibu wa Bwana Zitto Kabwe).
Sasa kulingana na tathmini nzima ya huyo Bwana Zitto Kabwe kuhusiana na suala la ujenzi wa Reli ya Kati linaleta walakini. Siamini kama huyo Bwana Zitto Kabwe haelewi zile taratibu mbalimbali za mikataba ya ujenzi na hasa ujenzi wa vitu vikubwa kama Reli. Huyu mtu anaelewa hizo taratibu na kama ni kweli hizo taratibu zimefuata basi hakuna sababu ya kuwa na mjadala wa mjenzi wa hiyo Reli awe ni nani na atoke Nchi gani. Kama ni zabuni ilikwishatangazwa na tena kwa uwazi bila kificho. Na makampuni mbalimbali ya kimataifa kutoka Nchi mbalimbali hapa Dunianai yaliingia katika mchanganuo wa hiyo zabuni ili kujipatia nafasi ya kushinda hiyo zabuni. Kama ilivyokuwa kanuni na taratibu za zabuni, ni yule mshindi wa hiyo zabuni ndiye atakayepewa jukumu la kuifanya hiyo kazi. Mshindi wa zabuni yoyote ile hapa Duniani iwe Tanzania ama Nchi nyingine yoyote ile hatokei hivihivi tu. Ni lazima awe amekidhi vile vigezo vyote muhimu vilivyotangazwa na yule mtoa zabuni. Na kwa bahati nzuri na inavyoonekana ni ile Kampuni ya Uturuki ndio ilijishindia hiyo zabuni na kwa uhakika kuwa ilikuwa na vigezo vyote muhimu na vinavyotakiwa kitaifa na kimataifa katika ujenzi wa Reli ya Kati. Sasa haya malumbano ambayo huyo Bwana Zitto Kabwe anayoyaleta yanatokea wapi.
ReplyDeleteAtueleza kwa kinagaubaga kama huo mkopo wa fedha za ujenzi wa hiyo Reli ya Kati ulikuwa na masharti kadhaaa na mojawapo ni hilo la kuwa maadamu huo mkopo wa hizo fedha unatokea China basi ni lazima hata kampuni ya ujenzi wa hiyo Reli ya Kati itokeee pale China kwa maana ya kwamba hata kama haikidhi vile vigezo vya mtoa zabuni basi na ipewe tu ilimuradi tusije kuharibu ule uhusiano wetu na huyo mtoa mkopo wa fedha (China).
ReplyDeleteSasa na kama ni hivyo je ni kwa nini hiyo zabuni iliitishwa kama sio upotoshaji na upotevu wa muda na fedha za walipa kodi walala hoi wa Tanzania. Ni kwa nini huo muda usingetumika kwa mambo mengine ya muhimu kuliko kuutumia vibaya kwa kukaaa na kuzichanganua hizo kampuni zilizowania hiyo zabuni kumbe ndani yake na nyuma ya pazia ilikuwa ni lazima hiyo kampuni itoke China. Ni kwa nini wasingeenda mojamoja na kuichagua hiyo kampuni kutoka China na kuipatia hiyo zabuni ili kuwafurahisha watoa huo mkopo wa fedha na pengine kurahisisha utoaji wa huo mkopo wa fedha na kuanza kwa ujenzi mara moja.
Kama nilivyowahi kuandika huko nyuma kuhusiana na huyo Bwana Zitto Kabwe ni mtu mnafiki na ni kigeugeu na ni mpotoshaji wa hali ya juu sana katika mambo mbalimbali yanayohusiana na mustakabali wa Taifa hili letu la Tanzania.
ReplyDeleteHuyo Bwana Zitto Kabwe ni mtu wa hovyo kabisa ambaye anatakiwa aangaliwe kwa jicho la tatu.
Huyo Bwana Zitto Kabwe anaelewa kwa undani athari za aina hiyo ya mikopo ya kuwafurahisha mabwana wakubwa.
Anaelewa kabisa athari za kuliruhusu jambo kama hilo katika nyanja mbalimbali ziwe za kiuchumi ama kisiasa. Kwa kuwaruhusu China kutuamulia sisi Watanzania ni kampuni gani ipewe zabuni ya ujenzi wa Reli ya Katika itakuwa inatuletelezea ule Ukoloni Mambo leo. Kitu ambacho kinatakiwa kipingwe kwa nguvu zote. Kama China inatoa mkopo na itoe. Kama ni kuwania hiyo zabuni ya ujenzi wa hiyo Reli ya Kati kutoka katika makampuni mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ufanywe na kwa kuzingatia vile vigezo vya kimsingi vilivyotolewa na Serikali. Kuruhusu mtoa fedha za mkopo kutuchagulia kampuni ya ujenzi wa Reli inawezekana kabisa wakatuchagulia ile kampuni ambayo haina vigezo vyovyote vile vya maana katika kukidhi haja ya huo ujenzi jambo ambalo ni la hatari sana na hiki kitu huyo Bwana Zitto Kabwe anakielewa. Kama Bwana Zitto Kabwe analichukulia kiwepesiwepesi suala la ujenzi wa Reli ya Kati eti katika misingi ya kudumimisha ule uhusiano madhubuti uliokuwepo baina ya Nchi hizi mbili za Tanzania na China na basi awachukue na kwenda kunywa chai nao jikoni.
Kama ni fedha za mkopo wazitoe na kama wana nia nzuri na Tanzania na sio kuvuka mipaka na kutuchagulia mjenzi wa hiyo Reli ya Kati. Kama ni hivyo basi ni bora waende na pesa zao.
Kuliruhusu jambo kama hilo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa hili la Tanzania kisiasa na kiuchumi. Hawa China ni kama wanataka kuuleteleza ule ukoloni mamboleo jamabo ambalo linapaswa kupingwa kwa nguvu zote kwani ni kama watakuwa wanatutawala sisi Watanzania.
Kama huyu Bwana Zitto Kabwe ana agenda zake nyingine anaweza kuzipeleka popote pale lakini sio kuzileta hapa Tanzania. HUYU BWANA ZITTO KABWE NI LOSER!!!!
wewe ni nani mbona kama unamshambulia ZITTO tu na vihoja vyako dhaifuuuu! kama umetumwa au una ugomvi na Zitto usituletee hapa hebu jaribu kufuatilia mchakato wa flyover ya Tazara labda utapata mwanga ktk hiyo ishu ya Reli.
Deletewewe ni nani mbona kama unamshambulia ZITTO tu na vihoja vyako dhaifuuuu! kama umetumwa au una ugomvi na Zitto usituletee hapa hebu jaribu kufuatilia mchakato wa flyover ya Tazara labda utapata mwanga ktk hiyo ishu ya Reli.
DeleteHoja hapa sio wewe ni nani. Hiyo ya wewe ni nani ama kama na ugomvi binafsi na huyo Bwana Zitto ama kama nimetumwa hizo ndio hoja dhaifu kwa taarifa yako. Mimi nimejizijibu hizo hoja za huyo Bwana Zitto Kabwe Mwanasiasa mwenye hoja dhaifu na za Kitoto ambazo sijapata kuziona katika Ulimwengu wa Siasa.Kama kuna suala la mchakato wa Flyover za Tazara mimi hilo kwangu silijui. Wewe lilete hapa likiwa limesheheni hizo critical analysis ili tulishughulikie. Kuzungumza hovyo hovyo bila kuzingatia misingi ya hoja za maana katika mazungumzo sio tu kuwa ni utoto bali hakutakusaidia kitu chochote. NDUGU NAKUOMBA UJIFUNZE KUWA NA CRITICAL THINKING AND ANALYSIS. WEWE PAMOJA NA HUYO MWANASIASA CHIBUKU NA DHAIFU ZITTO KABWE. ACHENI SIASA ZENU UCHWARA!!!
Delete"Namkumbusha Rais na Serikali namna ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani walivyovunja misingi yetu kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje, hasa kuhusu Sahara Magharibi na Mashariki ya Kati. Tumeikumbatia Moroko kwa ahadi ya viwanja vya mipira na misikiti na kuwaacha wananchi wa Sahara Magharibi ambao Mwalimu Nyerere aliwalinda kwa gharama zote."
ReplyDeleteHiyo misingi kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje inayohusiana na Nchi zilizopo Magharibi ya Sahara na Mashariki ya Kati ni ipi. Ni misingi ipi iliyovunjwa. Huyu Bwana Zitto Kabwe anatuletelezea ile namby pamby delusional approach ambayo haina nafasi kwa sasa na hasa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano. Anashindwa kuelewa kuwa this is the New Era!!!
"Sasa tunakwenda kuweka nyufa kwenye mahusiano yetu na China. Serikali ijitazame upya."
Na kama ni nyufa kati ya mahusiano ya Tanzania na China eti kwa sababu tu Watanzania na Serikali yao wamekataa huo aina ya ukoloni mamboleo wa kuamuliwa mambo yao basi na acha iwe hivyo. Ni bora kuzikosa hizo fedha na hayo mahusiano kuliko kuletewa kampuni ambayo kwanza sio tu kuwa haijakidhi vile vigezo vya hiyo zabuni achilia mbali haikushinda hata hiyo zabuni yenyewe. HUYO BWANA ZITTO KABWE NI MNAFIKI NA NI MTU WA KUOGOPWA KULIKO UKOMA!! NI MPOTOSHAJI MKUBWA SANA WA HABARI. INFORMATION ZAKE NI SO UNRELIABLE!!!!
WEWE ZITTO KABWE ACHA KUTURUBUNI SISI WATANZANIA. TUMEISHAKUSHTUKIA. WEWE NI MUONGO,MZUSHI NA MFITINA MKUBWA. UMEKUWA UKIENDA UKIKUZA MAMBO AMBAYO HAYANA KICHWA WALA MIGUUU!!!
ReplyDeleteJamani Mimi niliaha sema huyu mtu WA Kelemi Ni lazima arudishhwe kwao. Tumensaidia mpaka kumsomesha na Marehemu PIA alimfanyia msaada huo. Sasa anataka kuwa Mtanzzania aliyekosa Uzalendo. Ni bora arudishwe kwao. Tanzania yetu Ni ya. Watanzania na Ni watu wenye utanaduni wao na Upendso..wazalendo na tuna umoja ambao uko Katika danu zetu na DNA zetu. HUYU JITTO SI MWENZETU NA TUMENAHTUKIA ..KWAO MIREMBE NA TANZANIA YETU YA AMANI INAPETA. NA NI TANZANIA MPYA
ReplyDelete