Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema mwaka 2016 ulikuwa wa utumbuaji na majipu na kusahau kuongoza na kuboresha maisha ya wananchi.
Akizindua kampeni za chama hicho katika Kata ya Kijichi, Dar es Salaam, Zitto alisema Serikali inapaswa kuendelea mapambano dhidi ya ufisadi lakini pia kuimarisha hali za wananchi.
Akimnadi mgombea wa chama hicho, Edgar Mkosamali, mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema,“Sisi kama chama hatuna tatizo na mapambano ya Serikali dhidi ya ufisadi na rushwa, lakini ni vyema mapambano hayo yakaenda sambamba na kuimarisha hali za watu na hilo ndilo tatizo la walio wengi.”
Hakuna kilichosahaulika bwana ZZK ni mtazamo wako tu, hili "donda ndugu" la ufisadi lisipopona ni heri mguu ukatwe kuliko kuendelea kutesa Watanzania, machungu ya tiba yapo ndiyo hayo lakini tutapona, acha kulaumu, unga mkono mapambano.
ReplyDeleteHuyu Kijana mali zake alizotangaza. Ukijumlisha mali zake zoooteeee alizotanganza. Hata asilimia moja ya mali za aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadae Tanzania Mwl. Julius .K. Nyerere hazifikii za kwake. Achilia mbali mshahara na marupurupu anayoyapokea kwa kisingizio cha Ubunge. Huyu Kijana anamiliki mashamba na nyumba mpaka unabakia kushangaaa kama ni kweli kile anachokinena kutoka mdomoni mwake kina wiana na hali halisi ya matendo yake. Kimsingi nyie mnaojiita wapinzani tena wapinzani uchwara tumewashtukia. Hizo porojo porojo zenu dhidi ya Rais Magufuli ni hila tu. Ni zile hila zenu ambazo mnazificha lakini sisi Watanzania tumeishazigundua. Mh. Rais Magufuli amewashika pabaya na sasa mnabakia kutaharuki. Hamjui ile mikopo mliojikopa kwenye mabenki mbalimbali mtailipaje na mtairudisha lini. Kwa sababu mwisho wa siku mtafilisiwa hizo mali na mashamba mliojimilikisha na hizo mali zitarudi mikononi mwa Watanzania kama mimi ambao ni masikini wa kutupwa hata ekari moja ya shamba sina. Kwa kweli wewe Zitto Kabwe unayejifanya eti ni mtetezi wa Watanzania wanyonge ni muongo na pia una uzandiki na hila za hali ya juuu. Wewe Zitto Kabwe ni Adui namba moja wa maendeleo ya Taifa hili. Tueleze hizo mali zote unazozimiliki ni kwa nini na ni kwa manufaa ya nani kama sio ulafi na ufisadi na ubwanyenye na pia ukabaila. Mtoto mdogo kama wewe unajimilikisha mali zote hizo kwa tamaaa tu ambayo haimsaidiii chochote Mtanzania wa kawaida. Unajimilikisha mali kutoka Mtwara mpaka Kigoma. Unakopa mikopo ya Mabilioni ya shilingi kwenye mabenki ya walalahoi kama CRDB. Hata walalahoi hawawezi kukopeshwa hata shilingi moja licha ya kuwa hawajui hata mlo wao wa siku utatoka wapi. Wewe Zitto Kabwe pamaoja na wenzako mnaojiita kuwa ni watu wenye uchungu wa Nchi yetu ya Tanzania ni maadui wa kutupwa. Hatutaki hata kuwasikia. Mmekula na kuifilisi na kuifikisha Tanzania hapo ilipo. Tunataka kuona na wabunge wengine wanajitokeza na kuitaja ile mikopo pamoja na zile mali walizojimilikisha kwa tamaaa zao za fisi.
ReplyDeleteNa ndio maana nyie wabunge na wapinzani mmekalia kuja na hoja chungu mzima zisizokuwa na kichwa wala miguu za kuikosoa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na kumkosoa Rais Magufuli. Mara utasikia hii Serikali hivi hii Serikali vile. Sijui huyu Rais hivi sijui huyu Rais vile. Mara sijui operation Ukuta mara sijui vile. Yani ilimuradi tu kila kukicha mnakuja na hoja zenu dhaifu za kuikosoa Serikali. Kumbe ni katika hali ya uzandiki ule ule. Mnajua ni kitu gani hasa kilichojifija nyuma ya pazia. Kitu unachokifanya wewe Zitto Kabwe ni undumilakuwili wa hali juu ambao haujapata kutokea katika Nchi hii ya Tanzania. Pamoja na kelele zako zote kumbe ni mnafiki na mzandiki wa hali ya juu. Umejilimbikizia Mali pamoja na Hela ambazo hata hazihesabiki. Umejilimbikizia Mali kutoka Mtwara hadi Kigoma wakati wewe pamoja na kelele zako unajua kabisa kuna Watanzania wengi wao ambao ni masikini hawajawezeshwa hata kumiliki Robo Ekari ya Shamba. Leo hii bila hata ya aibu unakuja na hoja ya kuitaka Serikali kuwawezesha Watanzania ili kuboresha maisha yao. Swali ni je hiyo Serikali itawezaje kuyaboresha maisha ya Mtanzania mlalahoi wa kawaida wakati mtu kama wewe ambaye ni mbunge na ni mtu tunayetegemea kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kama kiongozi umejilimbikizia mashamba na mali nyingine pamoja na mabilioni ya shilingi zikiwemo maelfu ya fedha za kigeni/dollars??????......Wewe huyo ni Mbunge mmoja uliyejitokeza na kuanika ufisadi uliokuwa nao. Hatujui mambo yaliyopo nyuma ya pazia yanayowahusu wabunge wengine ambao kwa idadi inakaribia wabunge 300. Ndio maana kila kukicha mnapigana vikumbo pale Bungeni Dodoma kwa visingizio vya kutetea maslahi ya Nchi pamoja na Wananchi mnaowawakilisha. Kumbe ni uongo mtupu. Mko pale mnapigana vikumbo kwa maslahi yenu binasfi. Sasa sisi Watanzania tupo hapa tunasubiri kwa hamu kubwa kuona Wabunge wengine wajitokeze na kutueleza kwa kinagaubaga zile mali na mashamba pamoja na pesa wanazomiliki. Watanzania wenzangu mabibi na mabwana kwa sasa hivi TUKO VITANI. Hii VITA HAIMUHUSU MH. MAGUFULI PEKE YAKE. Hii ni Vita ya Watanzania wote na hasa wale walalahoi wa maisha ya chini. Hawa aina ya watu kama akina Zitto Kabwe na wenzake sio wenzetu. Na kwa kweli sio wenzetu kabisaaa. Hawa akina Zitto Kabwe wako Dunia nyingine kabisa. Na sio kweli kama wanavyodai kuwa wanaitakia Nchi hii ya Tanzanai mema. Hawa ni watu wako hapo kwa maslahi yao binafsi. Wako hapo kuyalinda maslahi yao yanayotokana na ufisadi wa kiwango cha hali ya juu ambao wamekuwa wakiufanya. Hawa akina Zitto Kabwe wameigeuza Nchi hii ya Tanzania kama Shamba la Bibi kwa maslahi yao binafsi na kwa visingizio mbalimbali vya kujifanya wanawatetea walalahoi. INATIA UCHUNGU SANA!!
ReplyDeleteKila kukicha hawa mabwana kazi yao ni kumkosoa na kumtukana Mh.Rais Magufuli pamoja na Serikali yake. Kumbe nyuma ya pazia kuna mambo maovu wanayoyapigania. Huyu Zitto Kabwe, Tundu Lissu na Lema na baadhi ya Wabunge wa CCM kazi zao ni hizo hizo za kuukosoa uendeshaji wa utawala wa Mh.Rais Magufuli. Lakini cha ajabu yale yaliyopo nyuma ya pazia na wanayoyapigania sisi Watanzania walalahoi hatuyajui na wala hayatusaidiii chochote. Kumbe wanachokipigania ni ule Ufisadi wao. Hawa Wabunge hata hiyo mishahara na posho mbalimbali wanazolipwa inatakiwa wakatwe ama zipunguzwe. Kwa sababu kwanza hizo posho na hiyo mishahara ya mamilioni wanayolipwa haiwasaidiii chochote Wananchi walala hoi wa kawaida. Ni jambo la kujiuliza kuwa tangu wameanza kulipwa hizo posho na hiyo mishahara ya mamilioni je imesaidia nini katika kuinua uchumi na pato la Mtanzania wa hali ya chini????......Bado tunaona mabarabara ni mabovu, huduma za jamii ndio kama hivyo za kusuasua, umeme bado ni wa shida, lakini cha ajabu ni kuwa hawa ambao inasemekana kuwa ni wawakilishi wa wananchi ama wabunge wamekuwa wakiendelea kunufaika kwa kujilipa mafao ya hali ya juu kiasi cha kuwa jeuri ya kumtukana Mh.Rais Magufuli na kutotiii ile mamlaka iliyopo madarakani. Jamani mwenye macho haambiwi ona. Hawa Akina Zitto Kabwe ni Mafisadi ambao hawatakiwi kuvumiliwa hata mara moja. Hawa ni watu ambao tunatakiwa tuwaangalie kwa jicho la tatu. Sio watu wa kuwaamini hata mara moja. Hiyo Mishahara pamoja na marupurupu mengine wanayojilipa inatakiwa ifanyiwe mapitio upya ili walipwe kulingana na kile wanachokifanya na hatimaye kurudisha nidhamu katika bunge.
ReplyDelete