ACT-Wazalendo Yamleta Tanzania Julius Malema


Kiongozi machachari kutoka chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Economic Freedom Fighter – EFF Bw. Julius Malema ni mmoja wa viongozi wanaotarajiwa kuwasili nchini kuhudhuria mkutano utakaondaliwa na chama cha upinzani cha ACT Wazalendo.

Mkutano huo unalenga kujadili mustakbali wa lililokuwa Azimio la Arusha.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam; Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo Bw. Ado Shaibu ametaja vyama vingine vilivyoalikwa na ambavyo viongozi wake wanatarajiwa kuwasili nchini kuwa ni chama cha Labour cha nchini Uingereza, Die Link cha nchini Ujerumani na Syriza kutoka nchini Ugiriki.

Shaibu amesema wakiwa nchini, viongozi hao watashiriki mjadala mpana wa maudhui ya lililokuwa Azimio la Arusha ambalo hivi karibuni ACT Wazalengo imeliibua upya na kuliita Azimio la Tabora, ambayo kimsingi maazimio yote yanazungumzia ujenzi wa jamii inayochukia rushwa na aina zote za unyanyasaji huku ajenda kuu ikiwa ni ujamaa na utaifa kwanza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad