Alichosema Kikwete Kuhusu Sakata la Dawa za Kulevya

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete, amefunguka kuhusu sakata la dawa za kulevya na kuipongeza serikali hususani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.

Kikwete amefunguka hayo leo katika kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, kinachoruka kila siku saa 11:00 alfajiri hadi saa 3:00 asubuhi.

Ametumia nafasi hiyo kuishauri serikali kuifikisha mwisho vita hiyo, ili kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa, huku akitolea mfano uwezo wa msanii wa Bongo Fleva, Langa ambaye kwa sasa ni marehemu ikidaiwa kuwa alipoteza maisha kutokana na dawa hizo, pamoja na shida alizokuwa akizipata msanii Ray C, za kutafuta dawa hizo hata usiku wa manane.

Ameitaka mamlaka mpya wa dawa za kulevya kuwachunguza watu 97 ambao majina yake yamekabidhiwa hivi karibuni na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na yeyote atakayethibitika kuhusika, achukuliwe hatua, huku akionesha imani kubwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Rogers William Sianga.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mhe, Ridhiwani nikweli kabisa lazima issue dawa za kulevya ifike mwisho kwani inawezekana, uwa nashangaa badhi ya wtu kuchangia katika mitandao kwa kujielekeza katika mapenzi yao ya vyama vya siasa badala ya kujadili tatizo linalozungumziwa.Vita hii itashinda kwakishindo kwa sababu wapiganaji wapo wa kutosha na hakuna atkayeonewa, ila atakayebainika basi sheria ichukuwe mkondo wake, majaji na mahakimu walioharibu kesi za dawa hizo maksudi kwa rushwa wafukuzwe kwa haibu. Kama suala la mahakama halitaimarishwa basi vita hii uenda ikashindikana kwani hakuna atakaye kuwa -convicted. Mahakama kilio hiki ni chenu na watanzania wanaangamia huku baadhi yenu wamejengewa maghorofa na wauzaji na wasmbazaji, haifai na hao wote hawatakiwi kukalia viti vya mahakama waende makwao.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad