Askofu Ajitokeza Kumtetea Mbowe Juu ya Issue ya Kuuza Madawa ya Kulevya..!!!


MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Viongozi wa Dini, Askofu Wiliam Mwamalanga, amesema amesikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kumtaja Freeman Mbowe kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Askofu Mwamalanga alisema kamati yao ilitilia shaka Bilicanas iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya Mbowe Hotels, kwamba ni moja ya maeneo yanayotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kufanya biashara zao, lakini si mwanasiasa huyo.

Alisema ukumbi huo wa starehe kuhusishwa na biashara hiyo, haikumaanisha kwamba mmiliki wake ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anahusika.

“Sisi tulisema klabu ya Bilinacas inajihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya kwa sababu walikuwa wanaingia watu mbalimbali ambao walikuwa wakiendesha shughuli hizo, lakini hatukumtaja mmiliki wake Mbowe ndiye anayejihusisha na dawa hizo,” alisema Askofu Mwamalanga.

Alisema kamati hiyo itashirikiana na Serikali ili kuhakikisha biashara ya dawa za kulevya inatokomezwa na wahusika wote wanafikishwa kwenye mikono ya sheria.

Kamati hiyo pia imempongeza Rais Dk. John Magufuli kumteua Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya mwenye taaluma ya kusimamia suala hilo, jambo ambalo limesaidia kutotajwa watuhumiwa hadharani badala yake wahusika waweze kuchukuliwa hatua.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee biashara ya madawa ya kulevya hasa cocaine na heroein haziwezi kuuzwa sehemu ambayo mwenye eneo hilo siyo member, anaweza hasijionyeshe moja kwa moja ila anajua kinachoendelea na anaye mwakilishi wake katika biashara hiyo. Biashsara hiyo ina fedha nyingi sana na inahitaji kuwa na moyo mgumu kukwepa mitego yake. Kutajwa yeye haiwezi kuwa ajabu,kwani yeye ni binadamu ana kichwa chake na anawaza yeye mwenyewe kama wanadamu, pia yeye kama binadamu wengine ni mdhaifu na ameubwa akiwa na doa la dhambi, ni hatari kumsemea mtu na ikija ikabainika ni kweli utasemaje? kna kipindi kwenye miaka ya 94, mtu mmoja mkubwa tu aliweza kusema mbele za watu kuwa JAVDA NI MWENZETU, tena kwa kujiamini, baadae alionekana siyo mwenzetu kwani alichukuwa fedha za nchi kuwa anaimarisha zao la katani kumbe fedha zote kavusha kwenda INDIA ama CANADA na yeye pia kutoroka nchi, wenye kufuatilia wanaliju suala hili, hivyo unahitajika kuwa muangalifu sana katika masuala haya kwani baadae unaweza kuunganishwa kuwa na weweunahusika na biashara hii.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad