AKIONGOZA ibaada katika Kanisa lake la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephati Gajima leo Jumapili, Feb. 12, 2017 amesema kuwa amemtumiwa ujumbe na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa akimpa pole mchungaji huyo na kuonesha kusikitishwa kwake na kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.
MAHUBIRI YALIVYOKUWA; IBAADA YA ASKOFU JOSE PHAT GWAJIMA KATIKA KANISA LAKE LA UFUFUO NA UZIMA;
Kwaya wamemaliza kuimba mzee wa kanisa anawapongeza na kusema “Kama Gwajima angeendelea kuwa ndani na wauza madawa kuendelea kutanua mtaani basi hii kwaya leo ingekuwa inamalizia kurekodi album yake pale central”
Gwajima ameingia madhabahuni ananena
“Mheshimiwa rais anapigana peke yake, kama kuna mtu ana mpango wa kunitenganisha na rais, atashindwa, huwezi kunitenganisha na rais.
Gwajima amewaombea Rais Dkt John Pombe Magufuli, Makam wa Rais, Bi Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadaye akamuombea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Gwajima: Nimeandikiwa meseji na DK Slaa
Askofu Gwajima baada ya kumaliza kuwaombea viongozi wakuu wa taifa amesema kuwa amandikiwa ujumbe kwa njia ya simu na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa.
“Baada ya kutoka polisi, viongozi wengi wa dini na serikali wamenipigia simu wakinipa pole lakini miongoni mwao ni Dk Slaa ambaye ameniandikia meseji.
“Sijajua yuko wapi, lakini ameniandikia ujumbe na nitausoma mbele ya waumini wote na Watanzania wasikie, sisomi huu ujumbe kwa ajili ya mambo ya kisiasa, la hsha nausoma ili kila niwaoneshe alichokisema Dk Slaa.”
UJUMBE WENYEWE
DK Slaa: Baba pole sana, pamoja na mengine yote, kwa hilo la madawa ya kulevya wamekuonea, hata kwa mali zako pia wanakuonea na kukudharirisha tu.
GWAJIMA: Nashukuru, nimepata meseji yak leo baada ya kuachiwa.
Dk Slaa: Mungu yuko pamoja nawe kwenye kweli, nilisema nitasimamia ukweli, na siyumbishwi, nipo tayari kukutetea. Mwisho wa kunakili.