Wakati vita dhidi ya madawa ya kulevya jijini Dar vikipanuka na kugeuka kuwa suala la kitaifa, kuna kila dalili kuwa usalama wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda upo hatarini, Risasi Mchanganyiko limebaini.
Juzi Jumatatu, Paul Makonda alijitokeza tena hadharani na kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yanayohusiana na vita alivyovianzisha, huku ikiwa ni mara yake ya tatu kutaja majina ya wanaojihusisha na madawa ya kulevya, safari hii, akitoa orodha ya watu 97.
HATARI YAKE IKOJE?
Biashara ya ‘unga’ ni moja kati ya biashara chache zenye fedha nyingi duniani, ambayo bahati mbaya inapigwa vita na serikali nyingi. Watu wanaojihusisha na shughuli hii, wana fedha nyingi na wako tayari kufanya lolote linalowezekana kuifanya biashara yao kuwa salama.
Kwa Paul Makonda kutangaza vita hadharani, tena akitaja majina ya watu na njia zinazotumika kuuleta, kuusambaza na kuusafirisha, anajiweka katika nafasi mbaya ya kuwa mlengwa wa wafanyabiashara hao, hasa kwa kuwa kukamatwa kwao siyo tu kutaharibu biashara yao hiyo, bali pia wao wenyewe watapotea.
Mfano mmojawapo wa jinsi watu wanaojihusisha na biashara hiyo walivyo na uwezo mkubwa, ni kesi ya bilionea wa unga wa Colombia, Pablo Escobar, aliyeuawa Disemba 2, 1993, baada ya mahakimu zaidi ya 30 waliosimamia shauri hilo kuuawa, licha ya kuendesha kesi hiyo wakiwa mafichoni, tena sauti zao zikiwa zimewekwa mawimbi ya kutofahamika.
MAADUI ZAKE WAMEONGEZEKA
Awali, ilionekana ni wauza madawa ya kulevya pekee ndiyo ambao wanaweza kusemwa kuwa ni maadui zake, lakini baada ya mazungumzo yake na vyombo vya habari Jumatatu iliyopita, watu ambao watafurahia kuona kiongozi huyo kijana anapatwa na matatizo, wameongezeka.
Watu hao ni pamoja na wamiliki wa maduka ya kubadilishia fedha maarufu kama Bureau de Change, wafanyabiashara wa mitungi ya gesi, wamiliki wa mahoteli na klabu za kamari (Casino), achilia mbali watoto wa viongozi wakubwa tokea serikali ya awamu ya tatu, chini ya Benjamin Mkapa.
KWA NINI HAWA?
Licha ya kushangazwa na wingi wa maduka ya kubadilishia fedha (alisema yapo zaidi ya 200 kwa Dar pekee), lakini pia aliyatuhumu kufanya miamala inayozidi kiwango kinachotakiwa kisheria, hivyo kuufanya mzunguko wa fedha zinazopitia hapo kuwa mkubwa.
Alisema wingi huo wa fedha, unatia shaka kuwa huenda unatumiwa na watu wa biashara ya madawa ya kulevya katika kutakatisha fedha. Kwa vyovyote, wenye maduka hawa hawajapendezwa na tuhuma dhidi yao na hivyo nao kuingia vitani kimyakimya.
Biashara ya mitungi ya gesi nayo ilitajwa kuwa ni mojawapo ya njia zinazotumiwa na wafanyabiashara hao kuficha madawa hayo wakati wakisafirisha kutoka au kwenda ughaibuni.
Aidha, alidai kuna hoteli kadhaa kubwa zenye wakazi wa kudumu, ambao wanatambuliwa na wamiliki wake, hivyo atahakikisha anawafanyia kazi, kitu ambacho kinaongeza idadi ya maadui, kama ilivyo kwa wamiliki wa nyumba 200 waliosemwa kuwa wanaruhusu biashara hiyo kufanywa ilhali wakijua ni kosa kisheria.
MBINU ZINAZODAIWA KUANDALIWA
Baadhi ya wanaharakati wanaopinga biashara ya madawa ya kulevya, ambao waliomba hifadhi ya majina yao, wamesema mbinu mbalimbali zinaweza kutumika ili kumdhuru kiongozi huyo, aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni.
Mbinu hizo ni pamoja na kumwinda na kumuua kwa risasi, kitu ambacho ili kukidhibiti, wameomba kuimarishwa kwa ulinzi wake, nyumbani, kazini na hata awapo barabarani.
VIDOSHO, AJALI ZA KUTENGENEZWA
Eneo lingine alilotahadharishwa kujihadhari nalo ni pamoja na wasichana warembo, kwani wanaweza kutumiwa na maadui ili kumtia matatizoni, ikiwemo kumwekea sumu katika chakula, kinywaji au hata kumdhuru kwa namna nyingine.
Wadau hao wamelitaja eneo lingine la hatari linalopaswa kuangaliwa zaidi, ni kwa maadui zake hao kuweza kumtengenezea ajali ya kumdhuru, ili mradi wafanikiwe kuzima harakati zake za madawa ya kulevya alizoanzisha na kuungwa mkono na watu wengi.
KUHUSU ULINZI, HUYU HAPA SIRRO
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alizungumza na Risasi Mchanganyiko juu ya ulinzi wa kiongozi huyo. Akionyesha mshangao, alisema suala hilo siyo jambo la kuuliza kwa sababu wao wanaelewa nini kinapaswa kufanyika.
“Tunajua ukubwa wa vita hivi na madhara yake pia tunajua, huyu ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, tunampatia ulinzi imara kabisa na kwa hili wala watu wasiwe na wasiwasi.”
Tunamwomba sana Mwenyezi Mungu Amwepushe na hayo mabaya yanayoonekana mbele yake Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Paulo Makonda, mpiganaji wa kweli wa watanzania. Atashinda kwa kuwa hayuko peke yake, anao wenzake ambao hawataki kurudi nyuma kutoka mstari wa mbele wa mapambano.
ReplyDeleteAmina.
Tunamwomba sana Mwenyezi Mungu Amwepushe na hayo mabaya yanayoonekana mbele yake Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Paulo Makonda, mpiganaji wa kweli wa watanzania. Atashinda kwa kuwa hayuko peke yake, anao wenzake ambao hawataki kurudi nyuma kutoka mstari wa mbele wa mapambano.
ReplyDeleteAmina.
Kwa bahati mbaya hao wauzaji wa dawa za kulevya wanataka kuchezamchezo wasioujua nini mwisho wake, wanaweza kufanya kama wanvyofikiri ila hata wao hawawezi kuishi kwa sababu kazi ya kupambana kwa sasa siyo ya upande mmoja tu ni vyombo vyote na watanzania wote ambao kwa wingi wanaunga mkono mapambano haya. Hakuna kulegeza kinachotakiwa sasa ni kuwatafuta kwa njia zote, za siri na za wazi na ikiwezekana kutoa uhai wa mtu ifanyike hivyo hakuna kulegeza kamba. Watu wakufanya kazi hii tena kwa miezi 6 tu wapo na wamejipanga kushinda vita hii. Kama kuna mtu anapinga au kubisha asubiri aone. Vitisho katika mapambano ni kitu cha kawaida kabisa na kitaalamu inaitwa psychological warfare, na inayo anti yake pia. Namkumbuka waziri wa mambo ya nje wa utawala wa hayati SADAAM HUSSEIN aliyejulikana kama AL-SAAFU aliwatikisa wamarikani wakati wa vita vya kumuondoa madarakani, lakini mwisho wake ulikuwa kama wamarekani walivyotakakuwa hata akijisalimisha ila lazima auawe. Hivyo tutegemee kila vitisho kutoka kila kona ila mwisho wa yote ushindi ni dhaili. Mhe, Makonda wewe ni Jabali usiogope kitu unalindwa na roho mtakatifu na vyombo vyote, YOU ARE WELL PROTECTED,anayetaka kujaribu ajaribu aone cha mtema kuni. ALUTA CONTINUA.
ReplyDeletejamani Watanzania...hasa wazazi..malezi ya watoto yamakuwa changamoto kwa ajili ya watu hawa wachache waroho wa fedha...hivi niwaulize hizo fedha mtazikwa nazo au?Wazazi wetu walitulinda tukawa watu wa kutegemewa...mbona tumeacha watoto na taifa letu liangamie?Ni Mtanzania yupi asiyejua au kuona madhara ya madawa haya kwa vijana wetu?Tumwogope Mungu na tushiriki kikamilifu kwenye vita hii kuanzia majumbani kwetu.tUSIONE HAYA kupeleka majina ya waathirika hata kama ni mtoto wako..ndiyo njia bora ya kumsaidia...kila mtumiaji na muuzaji ametoka kwenye familia Fulani...tuanzie majumbani kwetu tuwasaidie watoto.
ReplyDeleteNyuma ya Makonda wako wa-TZ wengi tunakesha na tunaomba kwa ajili ya nchi yetu,na bara letu,tunawaombea sana viongozi wenye nia njema na wananchi wao,na hakuna nguvu kubwa kuliko MUNGU.MUNGU TUNAOMBA UMLINDE PAUL MAKONDA.
ReplyDeleteWataua wangapi?? Mh. Makonda usiogope DUDU wala MENDE, MUNGU atakulinda inshallah, siku za hao MAHARAMIA kwa sasa ZINAHESABIKA..........'aluta continue'....HAPA KAZI TU
ReplyDeleteMUNGU AMSIMAMIE KWA KILA JAMBO ANALOFANYA KWANI ANAFANYA HIVYO KWA AJILI YA VIZAZI VYETU MAANA WENGI WAMEANGAMIZWA NA HAYA MADAWA YA KULEVYA. EE MUNGU WEWE NI MLINZI TOSHA.
ReplyDeleteMungu na amtetee,Vita hii ina ushindi kama tutamuweka Mungu mbele.
ReplyDeleteHii vita sio ya kawaida ni zaidi ya vita baridi ya urusi na marekani, Colombia afgastan na mexico wameshindwa pia hata raisi wa ufilipino kashindwa licha kuomba wampe wiki kadhaa lakin kachemka, mwisho kaamua kutangaza iwe vita endelevu
ReplyDeleteNa wao mwisho wao ni kifo,Na kwenda kuungua.
ReplyDelete