Burkina Fa­­so Mshindi wa Tatu Afcon 2017..!!!


Timu ya Taifa ya Burkina Faso imekuwa mshindi wa tatu wa mashindano ya Afcon yanayoendelea nchini Gabon, baada ya kuifunga Ghana 1-0 katika Uwanja wa Port-Gentil.

Mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Alain Traore katika dakika ya 89 uliomshinda kipa wa Black Stars, Richard Ofori ulitinga kimiani na kuifanya Burkina Faso kutwaa nafasi hiyo, ambayo Ghana imekuwa ikiitawala kwa muda mrefu.

Ghana ilitolewa na Cameroon katika hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kipigo cha 2-0, huku Burkina Faso ikiondoshwa na Mafarao wa Misri kwa njia ya mikwaju ya penalti.

Leo usiku macho na masikio yataelekezwa Gabon kushuhudia fainali ya kukata na shoka baina ya miamba ya Cameroon na Misri, mechi ambayo itaamua bingwa wa mashindano hayo makubwa zaidi barani Afrika.

Misri ni mabingwa wa kihistoria wa Afcon kwa kuwa wametwaa taji hilo mara saba, huku Cameroon maarufu kama Indomitable Lions wakitwaa ubingwa huo mara nne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad