Nyumba ya mama Wema Sepetu, Mariam Sepetu, iliyopo Sinza Mori jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia jana imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu.
Kutokana na tukio hilo viongozi wa Chadema wamechukua hatua ya kuweka ulinzi mkali nyumbani hapo na kuzungumza kuwa wamegundua kitu ambacho hawatakiweka wazi kwa sasa.
Baada ya tukio hilo kutokea mama Sepetu aliwasiliana na mwanae Wema Sepetu pamoja na viongozi wa Chadema, ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika na kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kuweka ulinzi.
”Tumeshaangalia mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira” amezungumza hayo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.
Meya alifafanua kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema bali hata nyumbani kwa Wema Sepetu ulinzi utaimarishwa kwani amegundua wanachama hao wapya wamekuwa wakiwindwa na watu wasiojulikana.
Wema alipohojiwa amesema, ” Mama yangu ameteseka usiku kucha kwa kukosa amani, amelia na kukosa hata hamu ya kula tumefika tumemkuta katika hali mbaya, najua yana mwisho ila tutazidi kufanya dua ya kumwomba Mungu atuepushie na mabaya yote,”.
Mama nae alihojiwa na kusema, ” sikuweza kutoka nje kwa kuwa najua mbaya wangu amekaa wapi na amekusudia kufanya nini,”.
Mama Wema wewe mtumzima baada ya kumukanya mwanao na wewe unafanya mambo ya kitoto. Hii siyo sababu yakuham chama kuna sababu nyingine.
ReplyDeleteMama wema na mwanae wote raia wa tz sasa meya pamoja na viongozi wa chadema mmeshatoa taarifa polisi?
ReplyDeleteCHADEMA?Yaani bora mngechagua chama kingine.
ReplyDeleteMimi chama pinzani chenye kupenda haki ni act wazalendo chadema ni walewale tu
ReplyDeleteNdiyo maana hata sasa tunakandamizwa watu jiiiii. Kwa hiyo ung'ang'anie chama japo huna amani?
ReplyDeleteKila mTZ anahaki ya kuabudu na kisiasa na ndiyo maana kuna wengine Siasa kwetu ukoma!!!
Kweli siasa mchezo mchafu. Hivi mnasubir tu mkidhani CCM ya Magu itatema kama zilizopita? Mtasubiri sana, na bora muanze kujishughulisha mapema.
Wasanii TZ maisha yao ni full of usanii na cheap. Watapiga kelelee kutafuta kiki CCM lakini watatupwa kapuni kama ilivyokuwa mwanzo.
Waandishi nao mshakuwa cheap. Kila MTU siku hizi anawapotezea muda? Au mmekuwa day care?
Yes in my opinion Wema amewahi sana, amekurupuka but all in all its her life!!! Nani humsaidia kila Siku? Wote huishia kumsema mitandaoni na her life goes on!!!