Dawa za Kulevya za Kigogo Mmoja wa Tanzania zakamatwa Nchini Kenya

Polisi wakimpelea mahabusu Mohamed Jabir baada ya ya kukamatwa na heroin katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Moi, February 2, 2017.

Polisi jijini Mombasa wamemkamata mwanaume mmoja akijaribu kusafirisha kilo moja ya heroin yenye dhamani ya Ksh 10 milioni kupitia Moi International Airport. Mwanaume huyo ametajwa kama Mohamed Jabir na alikuwa ameficha dawa hizo kwenye soli za viatu vyake.

Mkuu wa polisi uwanjani hapo John Otieno amesema mtuhumiwa alikamatwa Alhamisi iliyopita wakati akijaribu kupanda Rwanda Airways kwenda Dubai. Afisa mmoja wa polisi amesema kuwa dawa hizo ni za drug baron wa Kitanzania ambaye huwa anakuja na kuondoka mara kwa mara jijini Mombasa.

Mohamed Jabir amekamatwa siku chache baada Rais Kenyatta kutanga vita dhidi ya mapapa wa dawa za kulevya Mombasa. Tayari Mapapa wanne jijini Mombasa Baktash Akasha, Ibrahim Akasha, Ghulam Hussein na Vijaygiri Goswami wameshakamatwa na kuhamishiwa Marekani wanakohitajika kwa tuhuma za kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad