Diamond Akwama Kurejea na Zari Bongo...!!!


Msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaduwaza ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea baada ya kutua kutokea Sauzi akiwa peke yake, tofauti na ilivyotarajiwa kuwa angerejea na mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’.

Awali zilivuja taarifa kuwa, Diamond amekwenda Sauzi kumchukua Zari na mtoto wao aliyezaliwa hivi karibuni, Nillan ili waje kufanya sherehe kidogo.

Kufuatia taarifa hizo, Jumatatu iliyopita, nyakati za jioni, watu wa karibu na Diamond walifika ‘airport’ kuwapokea lakini kilichowashangaza wengi ni kumuona anatoka mwenyewe na mabegi yake, jambo lililowafanya wahisi kuna kitu.

“Hee, mbona yuko peke yake sasa? Zari na watoto wako wapi sasa? Au wamezinguana?” alisikika akisema mmoja wa akinadada waliokuwa uwanjani hapo.

Mbali na dada huyo, wengi walionekana kunong’ona kuonesha kutoamini wanachokiona na kwa kuwa Diamond alijua kuwa kawaangusha kwa kutokuja na Zari, hakuwa na mbwembwe zaidi ya kwenda kwenye gari lililokuwa limeletwa na kijana aitwaye Q Boy, wakaondoka zao.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waganda pia wanatuzidi maarifa huyu zari na wanaume wote hakuna aliye mnunulia nyumba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Wema kanunuliwa nyumba ngapi?

      Delete
  2. Waganda pia wanatuzidi maarifa huyu zari na wanaume wote hakuna aliye mnunulia nyumba diamond kaona kapendwa subiri ufeli ndio utajua

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad