Akiongea na waandishi wiki hii, Diva amedai wanaume ambao amewahi kutokana nao wanazungumza lugha hiyo ambayo amedai inamvutia sana.
“Sipendi mwanaume ambaye hajui kingereza, napenda kudate na mwanaume ambaye anajua kingereza,” alisema Diva. “Yaani imetulia na inapendeza kwa sababu siyo local local, wapo ambao waliwahi kunitokea lakini baada ya kujua hawajui kingereza nikawatosa,”
Alisema wanaume wake wengi anakutana nao kwa mara ya kwanza kupitia kipindi chake cha Ala za Roho kwa kuwa ndio sehemu ambayo atakutana na watu mbalimbali.
Mtangazaji huyo ambaye pia ni muimbaji wa muziki kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji ‘Heri Muziki’.
Huo sio upendo,ni ubaguzi na kama anaongea kitaliano ,au kifaransa ,niwanaume wangapi wanafundisha wake zao lugha na wanafanikiwa? Je wanaume wangekuwa na tabia kama yako dunia ingekuwa chungu,sijaipenda hiyo kama kioo cha jamii.
ReplyDeleteHuo sio upendo,ni ubaguzi na kama anaongea kitaliano ,au kifaransa ,niwanaume wangapi wanafundisha wake zao lugha na wanafanikiwa? Je wanaume wangekuwa na tabia kama yako dunia ingekuwa chungu,sijaipenda hiyo kama kioo cha jamii.
ReplyDelete