Fahamu Njia za Kupunguza au Kuondoa Kitambi Kabisa Bila ya Kunywa Dawa Wala Kufanya Mazoezi..!!!!


Uzito uliopitiliza ni upi?

Huu ni ule uzito ambao haufanani kiafya  na urefu wa mtu husika …

Njia rahisi ya kujua kama uko kwenye uzito sahihi ni hii.. mfano kama wewe una urefu wa sentimita 170.

Chukua 170 utoe 100 utapata 70. Kwa hiyo wewe hutakiwi kuzidisha kilo sabini.

Nb: 100 iliyotumika hapo ni costant.


 Zifutazo ni njia rahisi za kupunguza uzito

     Kunywa maji mengi kabla ya kula mlo wowote.

      Acha kula vitu vitamu sana vya kiwandani. Mfano, soda, pipi, biscuit na kadhalika.

     Usiingie kitandani kulala ukiwa umeshiba.

     Pata usingizi wa kutosha mfano  masaa nane na zaidi

     Weka chumvi kidogo sana kwenye chakula chako.

      Kula breakfast{chakula cha asubuhi} cha kutosha.

     Acha kula vyakula vinavyokaangwa na kuandaliwa haraka{fast foods}. Mfano chips, baga, saucage, vitumbua, maandazi, chapati na et.c

     Kula mboga za majani za kutosha i.e mchicha, Chinese, carrots, etc

   Kula matunda kwa wingi mfano apples, zabibu,

   Kula vyakula vyenye kamba{fibres} kwa wingi. Mfano kabechi, maembe, machungwa, machenza na etc

  jipangie ujazo maalumu mdogo wa chakula na ule ujazo huo kila siku, sio unakula huku unaongeza chakula ovyo.

   Punguza ulaji wa chakula aina ya wanga mfano ugali, mihogo, viazi vitamu,mikate na e.t.c

  Jipangie baadhi ya wiki unazimaliza bila kula nyama kabisa. mfano week moja kwa mwezi.

 Kula chakula aina ya protini kila mlo. Mfano maharage, karanga, soya, korosho, na kadhalika 

   Acha kushinda njaa kisha kula chakula jioni. Kula ata mara nne kwa siku ila kwa kiasi kidogo.

  Acha kunywa pombe kali eti  inakausha mafuta, hicho kitu hakipo na ni uongo mkubwa.

    Punguza unywaji wa bia i.e  kiafya mwanaume anatakiwa asinywe zaidi ya unit 4 za pombe  kwa siku na mwanamke anatakiwa asinywe zaidi ya unit 3 kwa siku.

Unit inapimwaje?

  Mfano bia moja  ina alcohol ya 8% ndani ya chupa lenye ujazo wa 500mils yaani nusu lita. Kwa hiyo ukinywa nusu ya bia{250mils} umefikisha unit nne tayari inabidi usinywe mpaka kesho tena kwa wewe mwanaume. Hivyo bia hiyo hiyo mwanamke hatakiwi kunywa  hata nusu yake.

   Kula chakula taratibu bila kua na haraka na hii husaidia mtu kula chakula kidogo na kuridhika. Mfano kula kwa dakika ishirini kila mlo.

Kwanini?

Mishipa ya fahamu ya tumboni inachukua dakika ishirini kugundua kama tumbo limeshiba hivyo na kutoa taarifa kwenye ubongo ili mtu aache kula. hivyo ukila ndani ya dakika tano ukamaliza, utahisi bado una njaa kwa sababu mishipa hiyo haijagundua kama umeshiba  hivyo utaongeza chakula kingine.kwa maelezo zaidi soma hapa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad