Gwajima Atema Cheche,Amtaka Makonda Amtaje Ridhiwani Kikwete Kwenye List Yake...!!!!


Gwajima: Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media?

Gwajima: Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii.

Gwajima: Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi;

1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi

2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya.

Gwajima: Nani anatakiwa kuniita mimi kama Askofu Mkuu Polisi? Ni Polisi sio Makonda. Makonda anajiona kama Mkuu wa Wakuu wa Mikoa yote na Mawaziri wote.

Gwajima: Sio desturi ya rais hata kidogo eti awatenge Mawaziri wake eti aongee na Makonda. Rais alikuwa anampongeza makonda kwa sababu kafanya Vizuri. Makonda anaujasiri na anajituma hivyo rais kumpongeza ni halali. Makonda anaweza kuwa Kiongozi Muu siku zijazo kama akiondoa baadhi ya Hitilafu.

Gwajima: Makonda angeweza kunipigia simu au Kuwagiza Polisi wakaniletea samasi au kuniita.

Gwajima: Nia ya Makonda ni kutaka jina la Gwajima liharibike. Kama Gwajima hafanyi na hajihusishi na Madawa ya kulevya watu wa Usalama wanajua. Nmefanya hii kazi ya Uchungaji kwa Miaka 20.

Gwajima: Si kweli kwamba makonda anatumwa na Rais Magufuli, rais ana tabia ya kupongeza saa nyingine anapiga simu Clouds kupongeza pale wanapofanya Vizuri.

Gwajima: Sisi tunamuunga mkono Mheshimiwa rais hata kama kwenye uchaguzi hatujamuunga mkono, Lakini kwa kuwa amechaguliwa yeye tunamuunga mkono

Gwajima: Naamin Makonda hajajificha kwenye "Usukuma" wake.

Gwajima: Namuomba rais amkanye Makonda. Chuki zake binafsi za mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye system ya Serikali, ni hatari sana

Gwajima: Makonda ni Mchapakazi lakini Mambo ya Utawala hawezi, namuomba rais amtafutie kazi nyingine, nashauri umtafutie kazi nyingine, sio umfukuze.

Gwajima: Chini yangu kuna Maaskofu 125. Kesho wataogopa nao watasemwa

Gwajima: Kuna siku Paul Makonda, Sitta na Mwakyembe walikuja kanisani kwangu hata CD ninazo na alihutubia hapa kwenye Madhabahu akinisifia sana, Leo ni kitu gani kimemfanya anichafue?

Gwajima: Je ikiwa Gwajima hahusiki, itakuwaje?

Gwajima: Mimi nlikuwa mkali sana juu ya utawala wa awamu ya nne. Miaka kwa miaka Tembo walikuwa wanakufa na hakuna hatua zilizokuwa zinachukuliwa.

Gwajima: Kuna Kipindi Ridhiwani Kikwete aliwapeleka Mahakamani Dr. Slaa na Mch. Mtikila akitaka wakanushe habari kuhusu utajiri wake, hiyo kesi sijui iliishia wapi.

Gwajima: Nani anamtumia Makonda?

Gwajima: Makonda ana nia ovu juu yangu na juu ya Wakristo. Anataka kuwaaminisha watu kwamba wokovu haupo.

Gwajima: Mimi nataka kununua ndege nyingine ili nianzishe chuo cha ndege, mbona sipongezwi kwa hilo?

Gwajima: Jambo hili alilofanya si sawa na si sahihi.

Gwajima: Wabunge wamepiga kelele juu ya jambo hili, sisi wananchi tusio na sehemu ya kuongea tufanyeje?

Gwajima: Namfahamu rais Magufuli, hawezi kumpendelea kwa kuwa ni mtu wa kwao (Msukuma). Rais anawapenda watu wote anawapenda Mawaziri wote na watendaji wote wa Serikali. Naamin rais hajamtuma Makonda.

Gwajima: Nguvu katika mikono isiyo sahihi ni hatari sana.

Gwajima: Juzi kati tulikuwa na mechi kati ya maasikofu na viongozi, Mimi nlikuwa namba tia yeye namba 10. Alikuwa ananiangalia jicho baya sana. Mimi, Makonda, kamanda Sirro Spika wa Bunge tulikuwa tunamechi si angenikamata hapo?

*Kuna watu walikuwa wanauza madawa ya kulevya, katika uongozi huu wale walikuwa wanauza madawa ya kulevya wamebadili majina na wanafanya biashara nyingine. Walikuwa na jina B sasa wamebadilisha jina.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo wewe mbona unataka kuchoma watu kwa chili zako binafsi..angalia yako na madini yanayotoroshwa halafu ndiyo vile.. Au umekuwa malaika sasa??

    ReplyDelete
  2. Akili fyatu huyu baba?"Mtumishi wa Mungu"??????
    Ona aibu.

    ReplyDelete
  3. Mchungaji wa kweli ni
    yule anaethubutu kutubu dhambi
    kabla ya kuanza kuihubiri INJILI.
    Mchungaji Donald Mwakisambwe amekiri kujihusisha na
    hii biashara haramu,katubu.
    Basi na wewe si utubu!Sema nilifanya madawa lakini nimeokoka,tutakuelewa baba.
    Wachungaji wangapi,maaskofu,mapadre,kwa nini utajwe wewe?MUNGU ANAKUONA.

    ReplyDelete
  4. Umechelewa mwambie Kashina was dawa za kulevya siyo Mhe. Makonda.

    ReplyDelete
  5. Haya mambo ni tata nadhani wanaomwamini Mungu waendelee kuomba ili inapotokea hali kama hii hekima ya Mungu iwe juu ya watumishi hawa. Ni kweli inastua kwa mhubiri kutajwa katika list ya waovu. Lakini tuiombee serikali ifanikiwe katika vita dhidi ya uovu, japo uovu una watetezi wengi, pia tukumbuke kuomba kwa ajili ya watumishi wote ili wajue jinsi ya kuendelea ( how to go about) inapotokea matatizo kama haya.

    ReplyDelete
  6. Vita dhidi ya uovu katika mahali ambapo uovu ni chimbuko, ni ngumu. dunia ni sehemu iliyojaa dhambi, sasa dhambi inapokemewa watu wanatuka na kupanga mikakati ya kuilinda dhambi hiyo. Dhamira ya mkuu wetu wa Mkoa ni nzuri sana, lakini sasa amezimishwa kana kwamba hakufanya kitu cha maana.
    Kwa askofu wetu kutajwa inauma lakini kwa nini tusisimame kuiombea serikali ifanikishe mambo yake ya kukomesha uovu? kama askofu wetu angemuombea mkuu wa mkoa, basi angakuwa ametimiza andiko la kugeuza shavu la pili kwa mtu aliye kupiga shavu moja.
    Tuiombee serikali na watumishi ili wakati huu wa kutetemeshwa kila kitu waweze kusimama. Amen!

    ReplyDelete
  7. Jamani hapa duniani ni nyumbani kwa uovu, ndio maana wanaotetea uovu ni wengi, uovu una wateja wengi kuliko wema. Tuiombee serikali na watumishi wa Mungu, watumishi wa Mungu tukumbuke kuiombea serikali kama biblia inavyosema (Warumi13). halafu kumbe kugeuza shavu la pili kwa mtu anayekupiga shavu moja ni ngumu tuko tayari kulipa kisasi kuliko kuweaombea wanaotuudhi. Hapa tumeshidwa kuendana na Neno la Mungu,Bwana Yesu atusaodie.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad