Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa atakayepokea rushwa kutoka kwa wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Taifa la kudhibiti dawa za kulevya nchini.
“Sheria ya udhibiti wa madawa ya kulevya itumike vizuri, Serikali na Baraza halitahitaji mtu yeyote mwenye mamlaka kupokea rushwa ikigundulika hatua kali zitachukuliwa,” amesema.
Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya udhibiti wa dawa za kulevya nchini ambayo yamekuwa yakifanywa na Serikali zilizotangulia