Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe, amepongeza jitihada za Rais Magufuli za kupambana na dawa za kulevya huku akisimulia alivyoshindwa vita hiyo wakati alipokuwa Wazri wa Uchukuzi, hususan katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam
Amesema alipata taarifa za kichunguzi kuhusu jinsi dawa za kulevya zinavyopitishwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, na akaamua kutangaza vita akisaidiana na mtu ambaye hajamuweka wazi, lakini mwisho mtu huyo aliyekuwa akiongoza vita hiyo, aliishia kufungwa gerezani mpaka leo.
Mwakyembe amesema hata baada ya yeye kutumia nguvu zake kumtoa gerezani ameshindwa, jambo ambalo linaonesha kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu kuliko kawaida, huku akionesha matumaini kuwa katika awamu hii, serikali itashinda.
Dk. Mwakyembe amezungumza hayo jijini Dar es Salaam, alipokutana na wahadhiri na wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa lengo la kupokea mapendekezo ya kanuni ya kusimamia sheria mpya ya msaada wa kupata msaada wa kisheria iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.
Watanzania wengi walikuwa wanajua kilichokuwa kinaendelea mhe, Mwakyembe, mtandao huo ni mkubwa na una watu weye uwezo na influence kubwa. Moja eneo ambalo wewe kama waziri ni kuangalia mahakimu na majaji wako, wengi uenda ni wazuri lakini wachache ni wabaya kuliko wachawi,wao wamekuwa ndani ya CARTEL za dawa za kulevya muda mrefu hata ukwasi waliokuwa nao unatisha sana, kesi za dawa za kulevya zimekuwa wakipewa wao na kuzimaliza kienyeji au kimya kimya kwa kushirikiana na polisi wasio waaminifu kuharibu vielelezo. Mahakimuna majaji waadilifu wanawajua na uchunguzi dhidi yao uanzie kwa majaji na mahakimu ndiyo watatoa muelekeo mzuri wa kuwafukuza kazi. Hawa watia doa kubwa taaluma ya sheria nchini. Bado mahakimu na majaji wameendelea kuleta vioja hasa mahakama za rufaa kwa kuwaachia majambazi sugu waliosumbua nchi karibu wote. Sina hakika kama hili mhe, unalijua, kuna wasiwasi ujambazi wa kutisha ukaanza tena kwa msaada wa majaji na mahakimu wasio waadilifu na waaminifu na wanjulikana wazi, kwanini majambazi waliohukumiwa maisha na vifungo vya miaka 30 wameachiwa na wapo huru wakati uhalifu walifanya? Tukio la majambazi kupora fedha ubungo kwenye mataa tarehe 20 April 2006 ambapo polisi aliuawa na mtunza fedha wa tawi la benki NMB -DAKAWA Mkoa wa Morogoro. Majambazi hao walikamatwa na kuhukumiwa kufa na wengine miaka 30, wakakata rufaa na wote wameachiwa huru, siyo hapa Dar hata Mza pia wameachiwa wapo nje. Kwanza hili vita hii ifanikiwe kwanza ni kuwafukuza kazi mahakimu na majaji wala rushwa wote kama alivyofanya Rais wa Nigeria jenerali Buhari, bila hivyo tunajisumbua na ni bora tuache tu.
ReplyDelete