Hivi Ndivyo Madawa ya Kulevya Yalivyomnufaisha Makonda Ndani ya Kipindi Kifupi Tu..!!!


Baada ya kuja na operesheni ya kupambana na dawa za kulevya, jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda linaweza kuwa ndilo lililotajwa zaidi katika mkutano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita na kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki ya pili sasa.

Makonda alianza kuwa mjadala ndani na nje ya nchi baada ya kutaja orodha ya kwanza na ya pili ya watu maarufu wakiwamo wasanii, wanasiasa na viongozi wa dini na kuagiza wafike Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam wahojiwe kuhusu dawa za kulevya.

Kasi ya kutajwa kwa jina lake iliongezeka zaidi Jumatano iliyopita baada ya kumtaja Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima na mfanyabiashara Yusuf Manji.

Hata hivyo, Mbowe, Gwajima na Manji wamekanusha vikali kuhusika na biashara hizo na kuahidi kumshtaki Makonda kwa kashfa. Gwajima na Manji wameshahojiwa polisi.

Katika mtandao wa kijamii wa JamiiForums, hadi kufikia juzi saa 8:00 mchana, kulikuwa na kurasa 49 ambazo jina la Makonda lilikuwa limetajwa mara 961 katika mijadala iliyokuwa ikiendelea.

Mijadala hiyo ilikuwa ikihusu kama Makonda yuko sahihi au la katika utaratibu alioutumia na kama ana mamlaka ya kuagiza watu kuripoti polisi.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hon, Makonda he is right, wangapi kati yenu mlithubutu kuwataja hao wauzaji na wasambaji wa madawa ya kulevya? huyu ni kiongozi na si mtawala, kiongozi anaongoza kwa mfano kama afanyavyo Makonda.Wauzaji wa madawa ya kulevya walitengeneza hali ya kuogopewa na kila mtu alikuwa akitolea mfano kwa marehemu AMINA CHIFUPA, aliyekuwa mke wa marehemu ABOUD MPAKANJIA, kuwa waliohusika na kifo chake ni wauza unga pale aliposma hadharani bungeni kuwa atawataja wauzaji na wasambazaji hata kama mumewe anahusika atataja tu. Wauza unga ni wahalifu wa kawaida kama walivyo majambazi na wachawi hata wanga. dawa mojawapo ya kuwashtua ni kuwataja kwa majina yao kama alivyofanya mheshimiwa makonda. Kinachofuata sasa ni strategy za kupambana na watu hatari wa aina hii. Kuna watu wanaweza kazi na ni wazalendo wa kweli kama alivyo Makonda na wanafanya kazi kwa kuweka rehani maisha yao na familia zao. Serikali iweke mfumo wa kuwapa kipaumbele walewote wakaoonekana kujitoa mhanga kwa ajili ya taifa lao na kuwapa heshima na kuwajali wakati wote. Mfano nani anaongelea kuhusu Amina Chifupa au kamanda NZOUWA katika vita hii? ningepata fursa ya kuonana na Mhe , rais ningemueleza kwanza kuwatambua watu hawa wawili na kumshauri kumuomba mstaafu kamanda Nzouwa aje kama mtaalam wakumsaidia kamishna Rogers aliyeteuliwa kupambana na dawa za kulevya.Nionavyo kama hakutakuwa na watu staili ya Kamanda NZOUWA vita hii uenda ikashindikana na hasa kwa hila. Pilivita hii ishirikishe vyombo vyote vya ulinzi na usalama kama ilivyokuwa wakati wa kupamabana na majambazi miaka 2006.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni Hemed mpakanjia sio abood mpakanjia

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad