Kamanda Sirro: Nasumbuliwa Sana na Wanawake Usiku


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, amesema miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni pamoja kupigiwa simu za vishawishi na wanawake hasa usiku wa manane, wakidhani anapata pesa nyingi kwenye kazi yake.


Kamishna Sirro afichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo, anajitahidi kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.


Amesema kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani, wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo wakati mwingine humpigia usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede.


"Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi". Amesema Kamanda Sirro


Sirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja na suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza  na mara nyingi huwa anachukua hatua.


Lingine ni uhalifu kuzidi katika eneo fulani na hufanya wananchi kuwa na uoga, na kupoteza imani kwa jeshi la polisi jambo ambalo linamfanya yeye ajisikie vibaya zaidi kuliko hata wananchi, huku nyingine ikiwa ni viongozi wa mitaa kutowajibika katika kudhibiti uhalifu pamoja na kuletewa
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kamanda si una mke?? Kama unaye waambie wanawake wanaokupigia simu wakampigie mkeo kabla ya kukupigia wewe.

    ReplyDelete
  2. Hivi ni haki kuiweka hii mtandaoni. Mbona hata sisi Wanawake tunafanyiwa hivyo. Lakini tunaona si profesional kuweka hii mtandaoni kutokana na maadili ya kazi zetu. Badala yake tunakwenda kwa mkuu kazini, au kiongozi fulani.Nashangazwa. Ni Wanawake ndio mnatudharalisha hivi, je Wanaume wangapi wanafanya hivi maofisini nasi hatuendi kuwaanika. Sisi wanawake tunahadhi p[ia.Watu wamemsema mama Sepetu, je tofauti gani. Kwa kiongozi wa juu kunukuu hii inanipa shida. Je hakuna Wanawake uliowapigia simu au kuwaomba kimapanzi. Je waje mtandaoni pia?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio muwache kutongoza wanaume.......hovyooo

      Delete
    2. Mbona povu?imepenya eeh?kwani hapo siro kakosea nini?Acha kutongoza.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad