Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Kumkamata Zitto Kabwe Bungeni

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe jana alijificha ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma  kwa hofu ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mara tu atakapotoka nje ya ukumbi huo.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika  kuwa Polisi wa bunge wamemwambia kuwa watamkakata kwa kosa la uchochezi ambalo yeye mwenye hafahamu ni lipi


 Zitto Kabwe Ruyagwa
And today it's my turn I've been informed by parliamentary security personnel that police will arrest me for sedition details are not known


Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa  amesema si kweli kwamba Polisi walikuwa Bungeni kumsubiri Zitto atoke wamkamate.

 “Hiyo taarifa yeye mwenyewe ndio anajitangazaia akamatwe lakini sisi hatumkamati kwasababu hatuna ishu nae

“Unajua watu wanafikia mahali wanatafuta umaarufu wakamatwe ili wapige mayowe… hatuna mpango wowote wa kumkamata kwasababu hajatenda kosa la jinai”  Amesema Kamanda Mambosasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad