Mamba Mla Watu Ziwa Victoria Auawa Kwa Kuwekewa Ndoano..!!!


Mamba anayesadikiwa kula zaidi ya watu wanane na kuendelea kutishia maisha ya binadamu na mifugo kandokando ya Ziwa Victoria katika Kata ya Mkuyuni jijini Mwanza kwa muda mrefu, hatimaye ameuawa baada ya kunaswa na ndoano iliyotegwa na wananchi kwa siku tatu mfululizo

Mamba huyo ameokotwa na wavuvi hii leo majira ya Alfajiri akiwa amekufa huku akielea juu ya maji katika mwalo wa mswahili uliopo mtaa wa Kang'ata kata ya Mkuyuni jijini Mwanza

Mamba huyo ambaye hakujulikana kama ni dume au jike, anakisiwa kuwa na urefu wa futi 18, sawa na mita tano na nusu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad