Manji Azidi Kutikiswa,Wafanyakazi Wake 126 Wakamatwa Haraka Haraka kwa Kukosa Vibali vya Kufanya Kazi Nchini


Upepo Mchafu Wazidi Kumuandama Manji, Baada ya Sakata la Madawa ya Kulevya kumuandama mpaka kufikia kulazwa Hospitalini, Uhamiaji nao wamekuja na Mpya baada ya kukamata Passport 126 ofisini kwake za watu kutoka nje ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yake bila vibali vya uhamiaji....

John Msumule ambaye ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam amesema, hii Kampuni ya Quality Group ipo katika jengo la Quality Center Barabara ya Nyerere kama unaelekea Uwanja wa ndege wa JNIA ni mkono wa kushoto. tumefanya kazi Ijumaa baada ya kuwekwa tu ndani yaani kesho yake jumamosi, tukapata Passport 126, Hizi ndizo zenye makosa. Tumechambua, passport 25 hawana vibali vya kufanya kazi, kwahiyo wanafanya kazi kinyume na utaratibu. Wote hawa hatua zitachukuliwa na watapelekwa Mahakamani.

Lakini lazima niseme ukweli, hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani, lazima Yusuf Manji ambaye ndiye mwajiri wa watu hawa ambaye ndiye Mmliki wa Kampuni hii lazima afikishwe mahakamani kujibu shitaka la kuajiri watu wageni wasio na vibali. Jana tulikuwa tumkamate alale mahabusu na leo ndio tumpeleke Mahakamani, Bahati mbaya tulipokwenda kumkamata, tukaapewa taarifa kwamba amelazwa Hospitalini hadi sasa.

Mara tu atokapo, aliport ofisi hii ili tumuunganishwe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali. Hatutajali ukubwa wa hela yako, hatutajali cheo chako cha mahali popote pale, hatutajali kwa njia yoyote ile una mamlaka gani katika nchi ya Tanzania.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Idara ya kazi iwashughulikie kwa kufanya kazi bila kuwa na vibali vya kazi.

    ReplyDelete
  2. kiukweli nashindwa kuwaelewa lengo lenu ni nini?

    ReplyDelete
  3. Illegal immigrants are prohibited. Illegal workers too. Tunataka kumkengea ajira mtanzania wakati wote. Sheria ichukue mkondo wake.

    ReplyDelete
  4. Huyo askari anaonekana hajui anachokifanya ni kama anafuata alichotumwa aseme bila ya kufanya homework kwanza.... this looks so personal ni nani anafuata sana huyu Manji na ni kwanini?? As far aso I remember Manji Alisha acha kazi quality tokea mid last year yaanI 2015.... what's going on jamani???

    ReplyDelete
  5. Huyo askari anaonekana hajui anachokifanya ni kama anafuata alichotumwa aseme bila ya kufanya homework kwanza.... this looks so personal ni nani anafuata sana huyu Manji na ni kwanini?? As far aso I remember Manji Alisha acha kazi quality tokea mid last year yaanI 2015.... what's going on jamani???

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad