Mbowe Aaachiwa Huru Polisi,Asisitiza Lazima Makonda Aisome Namba Mahakamani Leo..!!!


Hatimaye Jeshi la Polisi nchini limemwachia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe baada ya kumshikilia kwa saa 10.

Ofisa Habari wa chama hicho Tumaini Makene, amethibitisha kuachiwa kwa Mwenyekiti huyo ambapo pia amesema polisi wamemtaka kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kesho Jumatano.

Mbowe aliachiwa saa saba usiku wa kuamkia leo baada ya kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake na kukutwa ambako polisi hawakukuta dawa za kulevya zaidi ya nyaraka mbalimbali za chama zikiwamo Hati moja ya Chadema-Chaso kwenda kwa Mwenyekiti ya Julai 16, mwaka 2013, picha mbalimbali nane za matukio ya uhalifu, hati moja ya Rasimu ya Kwanza ya Chadema kuhusu uundwaji wa Red Brigade na hati moja ya kurasa 13 inayoongelea mambo ya Muungano.

Hata hivyo, pamoja na Mbowe kuachiwa na polisi Makene amesisitiza kwamba kesi yake aliyomfungulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja katika orodha ya wahusika wa dawa za kulevya iko pale pale.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbowe,hizi ni hatua za mwanzo na uhakiki na uoelelezi unaendelea. .. ushirikiano wako unahitajika. Kesho kitu LA usalama lipo kazini kuhakikisha Daresalamu yetu liko salama na nchi kea ujumla..zoezi linaendelea

    ReplyDelete
  2. Dah!Mkuu kwa hili hapana,kisasi cha nini?Kwani kuitwa kwa namna ya Makonda kumekupunguzia nini?Kama mtu huna dhambi ya kuhusu dawa za kulevya nilitegemea ungekuwa wa kwanza kuripoti polisi,na sio kukwepa kama ulivyofanya.Nyie viongozi wetu mnataka kuipeleka wapi hii TZ?Mmezaliwa,mmekuwa mmekuta amani kwa nini mnataka kufanya wadogo wasiishi kwa amani kama nyie?TAFAKARI.

    ReplyDelete
  3. nchi inaendeshwa kwa misingi na kumchafua mtu ni kosa mbele ya nchi zinazofuata mfumo wa utawala bora .... kila la kheri Mh Mbowe katika safari yako

    ReplyDelete
  4. Kinachoendelea ni visasi na kutafuta visheria vya ajabu ajabu ili kukomoana.Naamini hapo ni kwa kuwa aliyefanya huvi ni CCM,na aliyefanyiwa vile ni wa upinzani,hivyo kupelekea kuteteana kwa kuwa tu yule anatoka CCM.Igeni mfano wa Mh.Lowasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad