MBUNGE wa Simanjiro, James ole Millya (Chadema) amepongeza viongozi wa Serikali kwa jinsi wanavyojali na kuhudumia wananchi.
Alitoa pongezi hizo juzi kwenye mikutano miwili ya hadhara Orkesumet na Mirerani wilayani hapa, baada ya kupewa nafasi kusalimia wananchi kabla Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hajazungumza nao.
“Serikali hii ina viongozi wachapakazi akiwemo Waziri Mkuu. Kwa mara ya kwanza katika jimbo hili, wananchi watapata maji safi kupitia mradi wa maji kutoka Mto Ruvu unaoendelea kujengwa sasa,” alisema akiwa Orkesumet.
Alitumia fursa hiyo kumwomba Waziri Mkuu afuatilie ujenzi wa hospitali ya wilaya, kwani sasa wanategemea kituo cha afya na hali ikibadilika inabidi mgonjwa apelekwe Arusha Mjini umbali wa kilometa 150 kutoka hapo yalipo makao makuu ya wilaya.
Pia aliomba ijengwe barabara ya lami kuunganisha wilaya hiyo wilaya za Hai na Kiteto.
Akiwa Mererani, Ole Millya aliipongeza Serikali kwa kujenga barabara ya lami kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hadi Mererani. Hata hivyo, aliiomba Serikali iongeze juhudi ili barabara hiyo iweze kufika Mirerani na Orkesumet.
Akijibu maombi hayo, Waziri Mkuu Majaliwa alimpongeza Mbunge huyo kwa uungwana wake wa kutambua juhudi za Serikali kwa wananchi wa jimbo lake.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara, aliwaambia wakazi hao kwamba Serikali itaendelea kufanya nao kazi bila kubagua kwa itikadi za kisiasa.
Hii Serikali ni ya Tanzania kwa ajili ya Watanzania JPJM ameshatuambia yuko pale kututumikia bila kujali itikadi zenu salat vyama vyenu wala Deni na Amani Zenu wala Makabola Hebu.. Wekeni Anza nia kwanza .. Ni uzalendo na hizi ni ahadi alizotoa hapo amepitia mchana tawala lakini habagui wala hatobagua Ni Raising watu...Hapa kazi tu
ReplyDelete