MCHUANO Mkali Waibuka Kati ya Mawakili wa Chadema na Serikali..Kisa Hichi Hapa


Mvutano mkali wa kisheria umeibuka baina ya mawakili wa serikali na mawakili mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo – Chadema Freeman Mbowe katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa katika mahakama kuu na mwenyekiti huyo wa chadema dhidi ya mkuu wa mkoa wa dar es salaam Paul Makonda na wenzake wawili.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alifungua shauri la kikatiba No 1 mwka 2017 sambamba na hilo alifungua maombi ya kuimba makahama itoe amri ya zuio la kukamatwa, kushikilia na kuhojiwa kufuatia tuhuma zilizoelekezwa kwake na mkuu wa mkoa Paul Makonda za kujihusisha na dawa za kulevya.

Washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni kamanda wa polisi kanda ya dar es salaam kamishna Simon Sirro, na mkuu wa upelelezi wa mkoa wa dsm.

Awali akisoma hoja tano ambazo ziliwasilishwa na wapelekea maombi mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na jaji Sekieti Kihiyo, Pelegia Kadai na Lugano Mwandambo wakili wa serikali mkuu Gabriel Malata aliiomba mahakama kuu kutupilia mbali maombi hayo na kuyaita kuwa ni batili kutokana na kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikila kesi hiyo ambayo ameitaja kuwa ni ya kijanai wakati mahakama hiyo ina uwezo wa kusikiliza kesi za madai.

Hoja za mawakili hao wa serikali zinadai kwamba kisheria mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa zuio kwenye vyombo vya dola kwani maofisa wa jeshi la polisi wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria huku kikunukuliwa kifungu cha sheria y bunge kifungu namba 7 ambacho kinatoa malmlaka kwa mkuu wa mkoa
kumkamata na kumweka kizuizini mtu yeyote inapobidi.

Mawakili wa Bwan Mbowe wakiongozwa na Tundu Lissu na Peter Kibatala wamepingana na hoja za mawakili upande wa serikali na kudai kwamba mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi zinazohusiana na ukiukwaji wa haki za bianadamu hivyo walikuwa sahihi kuleta maombi hayo katika mahakama hiyo.

MARCHI 2 mwaka huu mahakama kuu itatoa maamuzi ya mapingamizi ya mawakili wa serikali dhidi ya mlalamikaji .

Wakati huo huo ameonekana akiwa miongoni mwa wapenzi wa karibu walioongozana na bwana Mbowe mahakama hapo huku kukiwa na taarifa kwamba anatarajiwa kujiunga na chama hicho kama anavyoeleza afisa habari wa chadema Tumaini Makene.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad