Meya wa Ubungo Amtaka Mbowe Kuwaruhusu Bavicha Kupambana an Polisi na Watawala,Amwambia Mbowe Wanangoja Amri Yake Tu Waanze Kazi..!!!


Dear 
Freeman Aikael Mbowe.

Salaamu na baada ya salamu,pole na mapambano ya kutufikisha "Canaan" kupitia ukombozi wa pili wa Taifa hili... Najua fika ujasiri na uimara wako wakati wote,sitishwi wala sijawahi kuwa na wasiwasi juu ya maamuzi na kila hatua unayopiga kuelekea mbele.

Ndiyo maana nipokuwa upande mmoja na wewe sitishwi na upepo wa kisulisuli,wala mvua za mabarafu,kwa kuwa najua ulivyosimama imara dhidi ya dhoruba na vimbunga,vya kusi na tonadozi

Walipokupokonya vitega uchumi vyako ulicheka huku mikono umeweka mifukoni,ukatuduwaza na kutuacha tukibubujikwa na machozi,walipokuja kujachufua hotel yako na ukwepaji kodi,ulituambia umechoka kuonewa huruma na kama hayupo tayari kukutana na haya tuachane na siasa za upinzani Africa,wiki baadae tunaona wamekufuata mpaka kwenye bustani za mchicha na nyanya,

Mimi na vijana wenzangu tulinyamaza kimya safari hii tukiogopa kufokewa tena na wewe,na baadae tulikumbuka maneno yako ambayo ulikuwa ukitusisitiza kuyakumbuka wakati wote. "Ni kweli wanaotutesa si wengi kama sisi tunaoteswa,ila kuingiza nguvu wakati huu no kihatarisha maisha ya wanyonge walioupande wetu,kwa nini tusisubirie watesi wetu wakiwa mahala salama kwetu,kuepusha maafa"

Na kwamba jeshi zuri si lile linaloshinda vita tuh,bali ni lile linaloshinda vita bila umwagaji damu na upotevu wa rasilimali zake nyingi,ingawa siku zote vita huacha wahanga.

Dear Freeman Aikael Mbowe,nasubiria kwa hamu command yako ya kusongambele,na nijaua si mimi tuh,nakuhakikishia vijana wenye utayari ni zaidi ya mamillioni,waona jeshi la adui lipo nje ya geti letu je na kuanza kuitikisa ngome yetu? Tuendelee kusubiria sauti yako kuu dhidi yao?

Vijana wako tupo tayari kukulinda kwa gharama yoyote hata kama ni damu na uhai wetu,ili makusudio ya ukombozi wa Taifa hili yafikie kama ilivuokusudiwa.

Marehemu mawazo,alipata kusema "wanaotudhalilisha na kututesa sana wanatuharakisha sana,kufika tunapo elekea"

Tabia za vyombo vya dolla ni zilezile tuh,kizazi na kizazi avitoamka na kuwa upande wetu milele

Je tuendelee kusubiria lingine zaidi ya hili au wakati ni sasa,? Askari wako Mtiifu
BONIFACE JACOB
senior councillor UBUNGO
MJUMBE KAMATI KUU CHADEMA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad