Mwanasiasa wa Uholanzi, Geert Wilders, anafanya mkutano wa mwanzo wa kampeni yake, na anahisi kuzuwia Waislamu kuhamia nchini humo, na kwamba atafunga misikiti.
Vilevile amawataja raia wa Morocco kuwa kashfa
Ulinzi mkali umewekwa katika mkutano huo karibu na Rotterdam.
Umebaki mwezi mmoja kabla ya uchaguzi, na kura za maoni zinaonesha kuwa chama cha bwana Wilders kina uongozi mdogo, ikilinganishwa na kile cha waziri mkuu, Mark Rutte.
Lakini katika majuma ya karibuni, wafuasi wa Bwana Wilders wamepungua.
Mwandishi wa BBC nchini Uholanzi, anasema kwa vile Bwana Wilders anamuunga mkono Donald Trump, inaonesha amepoteza baadhi ya wafuasi.
Chanzo: BBC
Wanasiasa wa bara la ulaya wanaweka mambo MATATU AU MANNE WAKATI WA KAMPENI ZAO ILIWACHAGULIWA.
ReplyDelete1.UTASIKIA HAWATAKI WAKIMBIZI NCHINI MWAO.
2.LAZIMA WALETE TUHUMA ZOZOTE JUU YA DILNI YA KIISLAMU.
3.WATAWATIA RAIA UOGA KUHUSU MAGAIDI NA KUDAI KUWA WATAKOMESHA UGAIDI.
4.WANAWEZA KUHALALISHA WATU WA JINSIA MOJA KUFUNGA NDOA.