Wanawake wawili wamekamatwa jana Jumamosi na kilo nne za cocaine nchini India. Wanawake hao wametajwa kama Pamela Devid Kiritta mwenye umri wa miaka 41 raia wa Tanzania na Thelma Mkandawire mwenye umri wa miaka 38 raia wa Zambia.
Wanawake hao wamekamatwa ndani ya hoteli moja iliyoko kusini mwa jiji la New Deilhi baada ya maafisa husika kutonywa kuwa walikuwa wanapeleka mzigo huo wa cocaine kwa mtu fulani. Mwanamke wa Zambia alisafiri na ndege ya kampuni moja ya Ulaya akitokea Addis Ababa. Maafisa hao walianza kumfuatilia mara tuu alipotua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa IGI.
Baada ya kucheki out, Mzambia huyo alichukua teksi na kuondoka zake. Maafisa walimfuatilia mpaka kwenye hoteli moja iliyopo eneo la Mahipalpur ambapo partner wake Pamela alikuwa anasubiria mzigo. Wote wawili walikamatwa kabla ya kuondoka hotelini hapo. Ndani ya begi la Mzambia kulikuwa na mzigo wa kilo nne za cocaine ambazo zilikuwa zimefungwa kwa ustadi mkubwa sana kiasi kwamba machine za airport hazikuweza kugundua.
Alipohojiwa na maafisa hao, Pamela alisema alikuwa amepanga kwenye flat moja iliyoko Vasant Kunj tokea Januari 20 mwaka huu. Pamela amesema kuwa alikuwa anamfanyia kazi mwanaume mmoja wa Afrika ya Kusini. Pamela ameitembelea India mara tisa tokea mwaka 2006. Pia Pamela ameshatembelea nchini nyingine kama Ecuador, Afrika Ya Kusini na Kenya. Maafisa wa India wanahisi kuwa safari zake zinahusiana na biashara ya dawa za kulevya.
Kwa upande wa Mzambia (Thelma) alikamatwa Pakistani mwaka 2015 kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Pia ametemblea nchi za China na Hong Kong kwa biashara hiyo hiyo.
yes like this is good hapo kwa hapo na ushahidi upo kabisa sio ya makonda kuita watu bila ushuhuda unawatia watu hatiani realese them what you're doing us not right at all
ReplyDeleteTobaaa
ReplyDeletewatanzania kwa kukamatwa na unga kumezidi, vipi yule aliyekamatwa na unga indoneisia amenyongwa au bado? alikuwa mtanzania
ReplyDeleteUnajuaje hana ushahidi?
ReplyDeleteHivi ushahidi unaweza kukosekana kweli kuwa Chid au TID wanatumia unga?
Wa bongo bana hapo kwa vile kaitwa wema ndio maana mnamsema makonda angeitwa mtu kama mimi wala msinge jali,,,acheni ujinga kwani waliopo jela wote mnahisi wana hatia??? Acheni mwisho wake ufike mbivu na mbichi zitajulikana kama hauzi au hatumii si atatoka tu,, na msilo lijua nikama usiku wa giza,,,,Kwa Taarifa Yenu WEMA IS A BIG DRUG DEALER,,,,,,,Ni chui aliye jivisha ngozi ya Kondoo na Ushahidi upo!!!!!
ReplyDelete