Timbulo amedai kuwa licha ya wimbo wake hivi karibuni kuvuja ikiwa na ID ya label ya QS Mhonda, haimaanishi kuwa amesainishwa na label hiyo.
Akiongea na Pride FM, Timbulo amedai kuwa wimbo huo ulirekodiwa kipindi ambacho walikuwa na makubaliano ya kufanya kazi pamoja na sio kusainishwa. “Siwezi kusaini na QS, sio label ya muziki ambayo mimi naiona inaweza kukuza muziki wangu,” Timbulo alimuambia mtangazaji wa redio hiyo, Eddy Msafi.
“Sio label ya muziki Tanzania ambayo inafanya hata muziki ambao unatakiwa Tanzania. Hawajui chochote kuhusu muziki, hiyo ni label ambayo labda wangekuwa wanafanya vitu vingine kama masuala ya ujenzi na vitu vingine kibao ambavyo mkurugenzi amesomea,” amesisitiza.
Hivi karibuni label hiyo ya QS Mhonda imeingia kwenye headlines kutokana na kuwa na ugomvi na Q-Chief aliyekuwa amesainishwa mkataba wa maisha. Chief amepigana hadi amefanikiwa kujitoa kwenye label hiyo kwa madai kuwa haikuwa ikimsaidia kwa lolote.
Yenyewe ilidai kuwa imetumia zaidi ya shilingi milioni 200 kwa Q-Chief lakini haijawahi kupata faida. Moja ya kitu kikubwa ambacho kampuni hiyo imefanya ni kumuanganishia collabo na msanii wa Nigeria, Patoranking ‘Koku’ ambayo inaonekana kama ilikuwa ni ya kupoteza muda. Wimbo huo ulivuja mtandaoni na kupotea ndani ya muda mfupi.