Mwigulu Nchemba Afunguka Ukimya Juu ya Sakata la Madawa ya Kulevya


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisimama Bungeni juzi, February 10, 2017 kuzungumza vitu mbali mbali vianavyohusu wizara yake ambapo aligusia kuhusu maswali anayokutana nayo kwamba kwanini hajaonekana akiongelea sakata la dawa za kulevya toka limeibuka Dar es Salaam.

Waziri Mwigulu alizungumza yafuatay:

“Lililoongelewa sana ni hili la dawa za kulevya, vita ya dawa za kulevya ni vita ya kila Mtanzania na haijaanza sasa, mimi tangia nilipofika nilikuta tayari Mh. Kitwanga ameshakamata Mapapa Wakubwa tu na tulivyotoka pale tumeendeleza.

“Ninachowaambia Waheshimiwa Wabunge tunaweza kutofautiana mtazamo kwenye approach na nyinyi kama Wabunge na Washauri wetu mkitushauri njia nzuri za kufanikisha jambo hili sisi mara zote tutakua tunapokea ushauri huo sababu vita hii ni yetu sote.

“Jambo moja tu ambalo nawahakikishia na ambalo nawaomba wote tuwe nalo, tusibadili lengo… na kuna watu wengine walikua wanasema mbona Waziri hujasema? ……..nimeshazunguka mikoa yote kasoro Njombe, Ruvuma, Singida na Songwe, kwenye mikoa yote huko nimetoa maelekezo ya kufanyiwa kazi, mojawapo ni dawa za kulevya.

“Nikishatoa maelezo kama hayo sibinafsishi tena hiyo shughuli, Mtanzania ambaye inamuhusu popote alipo lazima tusimamie mambo haya kwa upana wake, Waheshimiwa Wabunge katika maswala haya ya kitaifa tushirikiane wote, watu huwa hawagombani kwa ajili ya kazi watu huwa wanasaidiana kazi.” Alisema Mwigulu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad