Naibu Waziri wa Afya kuweka hadharani majina ya mashoga Dar es Salaam

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa atawaweka hadharani wanaume wote wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja (mashoga) ambao hufanya biashara hiyo kupitia mitandao ya kijamii.

Naibu Waziri aliyasema hao jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alieleza kuwa yupo katika ziara jimboni kwake na mara atakaporejea jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma rasmi ataiweka orodha hiyo hadharani.

Aidha, amesema kuwa wale wote wanaodhani kuwa vita dhidi ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni mzaha, wataona hali itakavyokuwa kwani vita hiyo ni kubwa sana na wataishinda.

Kigwangalla ambaye pia ni mtaalamu wa afya alisema kuwa suala la mtu kuwa shoga si suala la kibaolojia (asili) bali ni watu tu kujiendekeza na hivyo watakahikikisha wanalikomesha.

Sheria ya ndoa ya Tanzania inapinga watu wa jinsia moja kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, lakini pia ni kitu kilichozuiliwa katika vitabu vitakatifu vya dini.


Dr. Kigwangalla,
Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ushoga unaendelea. Watakamatwa kimya kimya! Serikali ina mkono mrefu. Wakipatikana watatusaidia wenza wao!

 Dr. Kigwangalla, 
Kuna watu wanadhani vita dhidi ya ushoga ni ya mzaha, ni vita kubwa na tutaishinda. Mtandao ni mrefu na nitaendesha operation kamata kamata!

 Dr. Kigwangalla, H.
Namalizia ziara jimboni. Nikirudi Dar, kabla ya kuhamia rasmi Dodoma, nitaweka wazi orodha ya watuhumiwa wa ushoga wanaojiuza mitandaoni!

 Dr. Kigwangalla, H.
Kuna nchi marafiki zetu zinafanya jitihada za kupenyeza ushoga Tanzania na kudai ni haki ya binadamu kuchagua ampendaye, sisi tunasema NO!

 Dr. Kigwangalla, H.
Ushoga hauna addiction wala siyo wa kuzaliwa nao, wanaofanya hivyo wanajiendekeza tu! Ushoga siyo biological. Mashoga wote waache mara moja

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad