Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku nne tangu mkuu huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya wakiwemo wasanii wa bongo fleva na filamu.
Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda, Babuu wa Kitaa n.k
Nape baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu suala hilo amesema kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.
Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.
Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.
Vimbele mbele wawili sasa kwaruzaneni wenyewe kwa wenyewe
ReplyDeleteTuache upotoshaji. Hakuna mahala katika statements zaNape amemtete Wema.Alichokisema Nape ni sahihi kabisa kuwa pamoja na kwamba anaunga mkono jitihada za kupambana na madawa ya kulevya pengine hakubaliani na namna zoezi linavyoendeshwa.
ReplyDeleteUkweli ulio dhahiri ni kuwa hakuna sehemu yoyote walishafanikiwa kutokomoza au hata kupunguza hii biashara kwa kutumia style ya Makonda. Zoezi hili kamwe hawezi kufanikwa kwa kwenda solo inabidi ashirikishe taasisi mbalimbali za kiusalama kwani mwisho wa siku mafanikio ya zoezi hili ni pale serikali itakapoweza kuangamiza network ya biashara hii kwa kuwatia ndani na kuwahukumu wahusika. Hili huusisha intelligence , legal ,etc ili kujenga kesi. Anachokifanya mheshimiwa Makonda ni ku stir mehemko ya watu na mwisho wa sk hakutakuwa na mafanikio yoyote.
Dog go nyum dog ina dis drug war
ReplyDeletehapo umenena nasio kwa ajili ya wema apana hayo unayoyasema hata mimi nakuunga mkono wauzaji na watumiaji wanajulikana sana huyu makonda sidhani kama anajua what he is doing na hocho cheo alichopewa it's too big for him hakiwezi he is jus pretending and acting mheahimowa Nape umenena tunapinga utumiaji na uuzaji kabisa sana tena lakini huwezi kumkamta au kumuita mtu kwa mahojiano halafu pale pale unawashikilia watu juat like that
ReplyDeletekwanza kwa nini uite watu ijumaa kama wewe huma chuki za ubinafsi nabkwa nini umwite petit nyumbani kwako halafu umpige then uite polisi waje wamchukue na utoe amri aendelee kupigwa nia yako nini? au leongo lako nini? hapa kuna walakin haiwwzekani wauza unga na watumiaji wa wanajulikana sana weww ulitaka tu kudhalilisha kina wema na petit na wengine lakini ujue na wewe yatakufika chozi la wazazi wao na dua zai hazipotei hata mimi nasema mungu atakuonyesha wewe mheshimiwa Nape kaongea sawa sawa you dont have proof you fobt know your work boy
ReplyDeletembona ray c hayumo kwenye list?
ReplyDeleteKichwa cha habari Na yaliyozungumzwa hayaendani.. Ape hajamtetea mtu. ILA anathibitisha kuwa hii Ni vita vyetu wote. Ni vya nchi mzima wewe Mimi yeye Na yule..tuamke sote nnchi Ni yetu Na wanaoathirika Ni wetu. Ni sisi WA kustopisha Na kukemea kwa njia zote. Kuanzia utendaji wetu katila mipaka Na ndani ya nchi..
ReplyDelete