NAPE Atoa Mkwala Mkali Mechi ya Simba na Yanga...Adai Ukikasirika Nenda Kavunje TV Nyumbani


February 23 2017 wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kuchangia Serengeti Boys Waziri wa habari, Sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye amezungumzia kuhusu mashabiki wataokwenda kutazama mechi ya Simba na Yanga Jumamosi hii February 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Waziri Nape amewashauri tu mashabiki ambao hawawezi kuwa na uvumilivu pale matokeo ya mechi yanapokuwa mabaya kwa upande wao “Jumamosi kuna mechi ya Simba na Yanga mtakumbuka mechi iliyopita kulikuwa na matatizo lakini nawaomba watanzania tuweke ustaarabu na uzalendo wetu mbele”

“Kama ukikasirika kunywa maji au nenda nyumbani, tunaomba tusiharibu miundombinu ya uwanja, Simba wanajua gharama waliyotumia kuukarabati uwanja ule, ukiona huna moyo wa kukaa uwanjani basi kaa nyumbani kwako angalia katika TV ukikasirika vunja TV yako” – Nape
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mkwala tu huo,na kuongea ruksa!wewe pia waweza kuwa sababu ya hayo unayoyaongelea,tangu niisikie video ya Nyerere na Mama Wema hakuna kuaminiana siku hizi.GOD BLESS TANZANIA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad