Mapema jana Mwanamuziki Khalid Mohamed maarufu kama "Top In Dar" (TID) ambaye alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuitwa polisi kwa mazungumzo ya tuhuma zake kuhusu anavyohusika na madawa ya kulevya, alifika nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kumsalimia na mazungumzo ya kawaida
Kwa muda wote ambao wawili hao walipokuwa pamoja walionekana kufurahia mazungumzo yao, wakiwa wamekaa kama marafiki. Mkuu wa Mkoa akitumia muda wa mazungumzo hayo kumshauri TID kuhusu maisha kwa ujumla na umuhimu wa kumtegemea Mungu katika kila jambo analofanya
Kwa upande wake TID yeye alitumia muda huo kumweleza Paul Makonda kuhusu maisha ya kawaida na yale ya muziki, Aidha, mazungumzo ya wawili hayo yaligusa kuhusu namna wanavyoweza kuokoa vipaji vya wasanii
Aidha, TID amenukuliwa akisema "Muziki bila madawa ya kulevya inawezekana... This is the turning Point kwangu mimi na kizazi cha muziki huu wa kizazi kipya, nikiwa na Mhe. Makonda leo tukijadili jinsi ya kuokoa vipaji na sanaa kwa ujumla, Mungu ibariki bongo fleva, Mungu ibariki Tanzania".
Naye Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika "Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tena nyumbani TID".