Petit Man Arudi Instagram na Ujumbe ‘Hatutaki Mazoea Kabisa’, Mashabiki Wampa Pole..!!


Mmoja kati ya watu 13 walioachiwa jana na mahakama kwenye sakata la Madawa ya kulevya, Petit Man amepost ujumbe wake wa kwanza katika mtandao wa Instagram huku akiweka sehemu ya wimbo wa msanii wake Billnass ‘hatutaki mazoea kabisa’.

Meneja huyo wa wasanii ndani ya label LFLG alikamatwa na jeshi la polisi mapema wiki iliyopita kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya pamoja na kutumia.

“Hatutakimazoeakabisa @billnass Feat @mwanafa #TurnOnComment #JahBless #LFLG,” aliandika meneja huyo Insta na kuleta mjadala mkubwa huku wengi wakimpa pole.

Petit Man, Said Alteza, Lulu Diva na wengine ambao walikuwa kwenye sakata hilo na kuachiwa na mahakama hapo jana, wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20 na watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa hao watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.

Huu ni ujumbe wa mashabiki hao wa Instagram.

nhappiness4
Toto nasikia ulipewa Mekong’oto wa haja hivi ni kweli da roho iliniuma kinoma

sherry_4real
Daah pole sn mshakaji wng ndo life ilivo cku azfanani kitu kidogo inaweza ikakuarbia siku au mwez pole sn dady yoo

florah_chiza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad