Picha: TID Aanza Maisha Mapya Baada ya Siku 5 za Lupango, Amtambulisha Mpenzi Wake Mpya..!!!


Msanii mkongwe wa muziki TID ameamua kusahau yaliyopita na kuanza maisha mapya ikiwa ni siku chache toka aachiwe na mahakama kwa sharti la dhamana ya shilingi milioni 10 na kutakiwa kuripoti polisi kwa mwezi mara mbili baada ya kukiri kutumia Madawa ya kulevya pamoja na wenzake 12.

Muimbaji huyo ambaye alikaa lupango kwa siku tano kabla ya kuachiwa, amemtangaza mpenzi wake mpya ambaye jina lake halikutambulika mara moja.

“The Smile i needed to see after all the trouble i have been through. Million Dollar Smile, am i in Love again!,”aliandika TID Instagram huku akaiwa ameweka picha ya mrembo huyo hapo juu.

Aliongeza, “Watasema sana na kisha watalala kama kunipenda najua unanipenda sana ooohyeahhh,”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad