Ridhiwani Kikwete Afafanua Kwanini ilikuwa ni Aibu Kwa TFF na Waziri, Diamond Kukabidhiwa Bendera Kwenda Gabon


Ridhiwani Kikwete aliingia kwenye headlines mwanzoni mwa mwezi uliopita pale alipoandika post Instagram akisikitishwa na kitendo cha Diamond kukabidhiwa bendera na Waziri wa michezo, Nape Nnauye kwenda kutumbuiza kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika, nchini Gabon.



Mbunge huyo wa Chalinze, amedai kuwa, post yake haikumlenga Diamond, bali aliwapa ujumbe shirikisho la soka Tanzania, TFF na Waziri Nape.


“Kilichonifanya niandike ile meseji ni baada ya kuona kwamba mashindano yanayoenda kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa miguu, lakini to our surprise, badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira wa miguu, tunawapa waburudishaji kwa maana ya wanamuziki kama Diamond,”
Ridhiwani alisema kwenye mahojiano na The Beauty TV.

“Matarajio yetu sisi ni kumuona kapteni wa taifa ndiye anayepokea bendera na sio wanamuziki,” ameongeza. “Pia watu wa TFF, kwamba nao wanashangilia yale anayoyafanya waziri?” Hivi vitu lazima tuwe serious.”

“Diamond yeye nampongeza sana, kwa hatua aliyofika, anafanya kazi nzuri, na ndio maana watu wamemuona, wamempa nafasi ya kwenda kutumbuiza ambayo sisi kama watanzania we feel proud. Lakini the bottom line ni kwamba, nini agenda kubwa inayomfanya Diamond aende Gabon? Ni mpira wa miguu, Diamond si mchezaji wa mpira wa miguu, hata kama labda anashabikia mpira wa miguu, lakini yeye ni mshabiki tu, wanaoenda kushiriki pale ni wachezaji.”

Ridhiwani amekiri kuwa kitendo hicho kilimsikitisha na ndio maana hakupenda kukaa kimya.

“Si kwamba sikupenda kwasababu amepewa Diamond, hapana, sikupenda kwa sababu, matarajio ya mimi mpenzi wa mpira ni kumuona kapteni wangu wa timu ya taifa anapokea bendera kwa niaba ya watanzania wote, anakwenda kutuwakilisha kule, hata kama tutashindwa, hata kama tutafanikiwa lakini anayetakiwa kwenda kule ni kapteni wa timu ya mpira wa miguu kwenda kutuwakilisha kama taifa na si vingine.”
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sioni huyo Ridhiwani alichokiongea sana sana anazidi kujichanganya tu, maana hata kama angepewa team captain angeenda huko kufanya nini wakati hatuna team tuliyopeleka? ni afadhali angesema team nzima ingekwenda kwa ajili ya kujifunza wenzao wanachezaje ili kupata mbinu za kupata ushindi. Diamond hakujipeleka huko ni team ya waandaji walimwona na kumpendekeza kwa ajili ya kuburudisha wakati wa ufunguzi, na ndo maana baada ya ufunguzi alirejea nyumbani. Nimwombe ndugu Ridhiwani kama kweli anataka soka letu lifike tunapotaka ni juhudi zake na za kwetu kuhakikisha team yetu ya Taifa inafanya vizuri ili siku moja ishiriki mashindano hayo na si kupiga kelele kwa ajili ya Diamond kukabidhiwa Bendera ya Taifa, hicho hakitatufikisha kokote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad