RIDHIWANI 'Kukamilika kwa Uchunguzi Kuhusu Biashara ya Dawa za Kulevya ni Ukombozi Kwangu'

Mbunge wa Jimbo la Chalinze na mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Ridhiwani Kikwete aonyesha jinsi gani anaumizwa na tuhuma za muda mrefu zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kwamba anahusika kwenye sakata la bishara ya dawa za kulevya.


Hivi karibuni mbunge huyo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio aliweka wazi namna ambavyo anaiunga mkono serikali katika vita ya dawa za kulevya.

Jumatano hii ameamua kurudi tena na kueleza jinsi navyoumizwa na kile kinachoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo.

“Ni jambo jema na la faraja kubwa kwangu kama uchunguzi unafanywa. Ni ukombozi kwangu, Ukweli utajulikana kuwa ni uvumi tu usiokuwa na chembe ya ukweli,” aliandika Ridhiwani Instagram.

Aliongeza,
“Ni maneno ya watu wasionitakia mema. Sina la kuficha. Sifanyi biashara hiyo haramu na wala sijawahi kufikiria kufanya. Ni bora kufa maskini kuliko kutafuta utajiri kwa njia hiyo,”

Uvumi huo umekuwa kwa kasi hivi karibuni baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kumkabidhi Kamisha wa kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga majina 97 ya watu wanaotuhumiwa kufanya biashara hiyo.

Mkuu wa mkoa huyo wakati wa kukabidhi majina hayo alidai wako vigogo wa biashara hiyo pamoja na watoto wa viongozi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lissu, usipotoshe watu. Zuio la muda maana take Ni nini? Mpaka ijumaa na polisi wanaweza kumwita wakitaka hivyo maana take Ni nini? Usipotoshe tafsiri za sheria. Stay of execution maana take Ni nini hapo umeomba utatafsiri kifupi jua wanao kusikiloza sio wote Ni wafahamu WA sheria..hapa kazi yu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad