Show ya Alikiba South Africa, Iwe Funzo Kwa Wasanii wa Bongo Fleva

Jana nyota wa Tanzania na Mshindi wa MTV EMA african act 2016 Alikiba alianza world Tour yake kwa showJijini Durban South Africa.

Kiwango cha idadi ya watu waliojitokeza na ukumbi aliofanyia show inathibitisha kabisa mziki wa bongo flava bado una safari ndefu kutoboa kimataifa hasa nje ya East Africa.

Collabo ni njia mojawapo ya kutoka kwenye nchi ngumu kama South Africa na Nigeria japo kuna baadhi ya mashabiki wanazibeza.

Sasa kama Alikiba na ukubwa wake huo amepata idadi hiyo ya watu, Billnass, Baraka da Prince au Timbulo atapata watu wangapi? Wakati chipukizi wa Nigeria Tekno akija bongo ndo main Artist.

Jionee picha za jana jijini Durban
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. nchi za wezetu ubaguzi ni mwingi kwa wageni au watu kutoka nje.wenyewe wanapenda kusamini vya kwao.sio sie kila kitu kutoka nje tunakumbatia .ndiyo hayo

    ReplyDelete
  2. Lkn kwa uono wangu mambo mengi ya kiba yanakuaga mabaya kwenye makala hii mazuri machache sana kila kitu mnambeza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeonaeeh!! Hata mimi naona hivyo-hivyo, mambo ya Kiba, Makonda na CCM yake kwa ujumla katika blog hii yana-andikwa kinyume-nyume, tofauti na mambo ya watu wa vyama vingine hasa chadema, hata kama kitu hakina maana watakipamba mpaka basi....... nadhani wanajichosha tu, ukweli-utabaki-kuwa-ukweli-daima!!

      Delete
  3. siku hazifanani jaman hata biblia inasema kila jambo na wakati wake kuna wakati wa kupata na wakkati kukosa wakati wa kulia na wakati wa kukosa wakati wa kukumbatia na wakati wakuto kukumbatia sema binadamu tukikosa kitu huw tunalalamika sana tushukuru kwa kila jambo ukipata ww mwenzio kakosa na ukikosa ww mwezio kapata ndivyo dunia inavyokwenda sasa eti ooh iwe funzo kwa wengine kwa kipi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad