Simba inaonekana haitamuachia kiungo wake Said Ndemla kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Sweden.
Taarifa kutoka ndani ya Simba, zinaeleza kwamba uongozi wa klabu ya AFC inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden anakocheza Thomas Ulimwengu haujawa wazi sana katika maelezo yake.
“Unajua wamesema wanamtaka Ndemla, lakini hakuna maelezo ya kutosha na ku
eleza biashara hii inafanyika vipi,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.
“Wanamtaka, Simba inapata kiasi gani? Inafaidikaje sasa na baadaye? Maana isiwe mnakuza wachezaji halafu watu wanaingiza maneno mengi wanakwenda kufaidika wao.
“Hatuna shida na kuachia watu lakini tunachotaka ni uhakika wa mambo. Simba tumeumizwa sana na hata hapa Tanzania imekuwa hivyo. Tunasumbuka kuwakuza, halafu faida kwa wengine, hii sis awa.”
AFC imeonyesha nia ya kumtaka Ndemla lakini taarifa zinaeleza wameshindwa kulipa chochote zaidi ya kusema wamchukue halafu baadaye wakimuuza, Simba itafaidika pia.