SMZ Yachachamaa Matokeo Mabaya Shuleni..!!!


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuna tatizo katika usimamizi wa elimu visiwani humo kiasi cha kusababisha kuwapo kwa matokeo mabaya kila mara.

Hayo yamesema na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alipokutana na viongozi wa shule na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.

Balozi Idi amesema kamati za shule zina jukumu la kuondoa hali hiyo kwa kuwabana walimu kila wanafunzi wanapofanya vibaya ili waweze kupandisha kiwango cha ufaulu.

Amesema, kamati hiyo zinatakiwa kuwaita walimu na kuwaweka ‘kitimoto’ waeleze sababu badala ya kuwaangalia wakati jahazi la elimu linaporomoka.

Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar amesema matokeo mabaya ya mitihani ya wanafunzi yanadhihirisha usimamizi mdogo wa walimu shuleni ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Hata hivyo, Waziri wa Elimu, Riziki Pembe Juma amesema pamoja na kuwapo kwa mikakati mbalimbali ya kiserikali kuinua elimu, wazazi wana nafasi yao kufanikisha suala hilo na kwamba, walimu peke yao hawawezi kufanikisha.


Riziki amewahamasisha wazazi na walezi kila mara wajitahidi kufuatilia mienendo ya watoto wao kuanzia shuleni hadi majumbani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad