Spika Ndugai: Makonda ni Mtani Wangu, Hivyo Msijali Maneno yake

Bila shaka hili ni dongo zuri kwa Makonda, na ni sawa na kusema watu wayapuuze maneno anayoyaongea kwa kuwa ni utani tu

Siku moja baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutakiwa kutimiza ahadi yake ya kuweka vifaa vya kupima wabunge kama wametumia kilevi ama dawa za kulevya kabla ya kuingia Ukumbi wa Bunge, amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni mtani wake, hivyo watu wasijali maneno yake. Aidha, katika Mkutano wake uliofanyika juzi, Makonda alimuomba Spika Ndugai kuweka kipimo hicho ili kabla wabunge hawajasimama kuchangia hoja wabainike kama wanatumia dawa za kulevya au la.

Chanzo: Dar24
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad