Kiungo wa kimataifa wa Ghana aliyekuwa akiichezea timu ya Arsenal ya England kuanzia Academy na mwaka 2011 kupandishwa kucheza timu ya wakubwa Emmanuel Frimpong, amejiunga na timu ya AFC Eskilstuna iliyopanda Ligi Kuu Sweden msimu huu.
Emmanuel Frimpong amejiunga na AFC Eskilstuna ambaye wiki kadhaa nyuma mtanzania Thomas Ulimwengu alijiunga nayo pia kwa mkataba wa miaka mitatu, baada ya kumaliza mkataba wake wa TP Mazembe na kutotaka kuongeza.
Frimpong anajiunga na AFC Eskilstuna ikiwa ni siku chache zimepita toka avunje mkataba na timu ya Arsenal Tula ya Urusi, ambapo katika msimu wake mmoja alikuwa hatumiki sana na alipata nafasi ya kucheza mechi tatu kwa mujibu wa mtandao wa ghanasoccernet.com
AFC Eskilstuna inaonekana kudhamiria kuleta ushindani katika Ligi Kuu Sweden inayotarajia kuanza mwezi March, Frimpong alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya vijana ya England U 16 na amekulia katika Academy ya Arsenal kuanzia 2001-2011 alipopandishwa timu kubwa na kuichezea hadi 2014.