Trump Amfanyia Umafya Waziri Mkuu wa Australia,Amkatia Simu na Kuutukana utawala wa Obama Kwenye Twitter..!!!


RAIS Donald Trump wa Marekani amemkatia simu Waziri Mkuu wa Australia, Malcolm Turnbull wakati wakizungumzia makubaliano ya nchi hizo juu ya wakimbizi.

Mawasiliano hayo ya simu kati ya Rais Trump na Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya kuwachukua wakimbizi.

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo.

Bwana Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini Marekani.

Australia imekataa kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na Iraq na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea.

Waziri mkuu Turnbull amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi kuingia nchini Marekani.

Bwana Turnbull baadaye alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.

Alikiambia kituo kimoja cha redio mjini Sydney kuwa ripoti kwamba Trump alikata simu si za ukweli

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad