Uchokozi: Korea Kaskazini Yaifyatulia Kombora Japan


Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena imefyatua kombora na kulielekeza upande wa Pwani ya Japan. Maofisa wa kijeshi kutoka Korea Kusini wamekadiria kombora hilo limesafiri umbali wa takribani kilomita 500 huku serikali ya Korea Kusini sasa imeitisha kikao cha kiusalama mjini Seoul .

Maafisa wa Pentagon nchini Marekani nao wamesema wamelifuatilia tukio hilo na kuongeza kuwa wamebaini ni kombora la masafa ya kadri.

Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini amesema vitendo kama hivyo vya uchokozi unaoendelezwa na Korea Kazkazini vinaonyesha dhahiri jinsi utawala jirani yao huyo usivyo na makini huku wakipania kuwa na zana za Nuclear.

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe ambaye angali ziarani Marekani, ameshtumu ufyatuaji huo wa Kombora huku Rais Trump akimhakikishia Abe kuwa anamuunga mkono asilimia 100.

Harakati hizo za ufyatuaji wa kombora zimekuja siku moja tu baada ya mazungumzo kati ya rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe mjini Washington, ambako wamekubaliana kulipa kipa umbele swala la jinsi ya kukabiliana na vitisho vya zana za kinuklia kutoka Korea Kazkazini..

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad