Ukiegesha Kiholela Gari Lako Dar, Adhabu Hii ni Halali Yako..!!!


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jafo, amesema serikali haitasita kuchukua hatua kwa wote watakaokiuka utaratibu za maegesho ya magari katika jiji la Dar es Salaam, kwasababu kufanya hivyo ni kusababisha msongamano na kero kubwa kwa wengine.

Ufafanuzi huo umetolewa na naibu huyo wa waziri, mjini Dodoma katika mkutano wa sita wa Bunge. Akitoa ufafanuzi juu ya hatua zitakazochukuliwa na serikali juu ya watu wenye maduka wanaopaki magari yao kwa muda mrefu, alisema, “Sheria ndogo ya maegesho ya magari GN namba 60 ya mwaka 1998 kifungu cha (6) kifungu kidogo cha (1) inaipa mamlaka ya halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kudhibiti na kusimamia maegesho ya magari yaliyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ili kuondoa kero, usumbufu na msongamano katika mitaa na katika barabara za umma. Kwa mujibu wa sheria hiyo maegesho yote ya magari ya kulipia na maegesho yaliyohifadhiwa yatumike kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, baada ya muda huo maeneo hayo huwa huru kwa matumizi ya umma pale inapobainika mtu kuhodhi maeneo hayo baada ya kumi na mbili jioni, halmashauri ya jiji huchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Aliongeza, “Kazi ya ukaguzi na udhibiti na maegesho imetolewa kwa mawakala katika jiji la Dar es Salaam, napenda kutoa wito kwa wamiliki wa magari kuacha kuegesha magari bila utaratibu hasa wakati wa usiku na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine. Serikali haitasika kuchukua hatua kwa wote watakao kiuka utaratibu za maegesho ya magari katika jiji la Dar es Salaam, kwasababu kufanya hivyo ni kusababisha msongamano na kero kubwa kwa wengine.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad