Wabunge Wacharuka Matumizi ya Fedha za Wafadhili...!!!


Wabunge wameitaka Serikali kutoa maelezo ya Dola 300 milioni za Marekani  (sawa na Sh570 bilioni) zilizotolewa na wahisani kusaidia miradi ya afya, lakini hazijatumika.

Fedha hizo zilitolewa na Global Fund kugharimia miradi ya ukimwi, malaria na kifua kikuu (TB) na zinatakiwa hadi Desemba mwaka huu ziwe zimeshatumika.

Mjadala huo ulizuka jana katika semina ya wabunge wa kamati tatu za Bunge kuhusu afya ya wanawake, watoto na vijana iliyoandaliwa na Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU) na Bunge la Tanzania.

Semina hiyo ilishirikisha Kamati ya Bajeti,  Huduma na Maendeleo ya Jamii na ya Masuala ya Ukimwi.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alisema bila kuwa na bajeti ya kutosha, malengo ya pambano dhidi ya ukimwi hayawezi kufikiwa.

“Tunasikia kuna wadau wengi waliokuwa wanasaidia eneo hili wamejiondoa. Nataka kufahamu wanasemaje kuhusu hili?” alihoji.


Akijibu hoja hiyo, Marianna Balampama kutoka Kundi la Washirika wa Maendeleo (DPG), alisema wafadhili hawajajitoa kusaidia miradi hiyo.

Balampama alisema Marekani na Global Fund wanaendelea kutoa misaada na kwamba, muda wa matumizi ya fedha zilizotolewa na Global Fund unakaribia kuiisha na hazijatumika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad