Rapa Nikki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi ameungana na rapa Nay wa Mitego kusema kuwa baadhi ya wachungaji wa makanisa hivi sasa wamefanya makanisa kama biashara na kujiingizia kipato.
Kwa upande wake Nikki wa Pili anasema wachungaji wanajua sana biashara kwa kuwa wanajua mahitaji ya watu kulingana na wakati jambo ambalo huwafanya wachungaji hao kuja na maombi ya kitu ambacho huenda wakati huo ndiyo hitaji kubwa kwa walio wengi hivyo ni lazima watu wenye hitaji hilo waweze kufika katika madhehebu hayo.
"Maombi ya kuombea waliokosa waume..wachungaji wanajua biashara sana..wanacheza na mahitaji ya soko" aliandika Nikki wa Pili
Mbali na hilo Rapa Nikki wa Pili amefunguka na kusema katika muziki hakuna kitu kinaitwa kubebwa bali unatakiwa kufanya kazi kwelikweli ili kuendelea kuwa katika ramani ya muziki kwa muda mrefu, kwani yeye anakaribia kufikisha miaka 10 na hiyo ni kutokana na jitihada zake na kufanya kazi kwa kujituma zaidi.
"Januari mpaka sasa nimesharekodi zaidi ya nyimbo 10, G Nako Warawara amerekodi zaidi ya nyimbo 20 labda ndiyo sababu nakaribia kufikisha miaka 10 kwenye game, muziki hauna bahati wala kubebwa fanya kazi" alisema Nikki wa Pili
uko vizuri kijana! wasanii wanaolilia kwamba fulani anabebwa ni wavivu wa kufikiri. Jitume, tengeneza kitu kizuri, cheza na soko!
ReplyDelete